Friday, September 15

Myanmar yatakiwa kukoma kuwatesa Waislamu wa Rohingya

Waislamu wa kabila la Rohingya wanaowasili nchini Bangladesh inadaiwa kuongezeka maradufuHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWaislamu wa kabila la Rohingya
Kiongozi wa wengi katika bunge la senate nchini Marekani, Mitch McConnell, amesema kuwa kiongozi wa Burma Aung San Suu Kyi amemwambia kuwa anakubaliana na haja ya kuwaruhusu zaidi maafisa wa kutoa msaada kwa Waislamu wa kabila dogo la Rohingya na amechukuwa jukumu la kuhakikisha hilo linafanyika.
Amesema katika mazungumzo ya simu bi Aung San Suu Kyi kadhalika amesema ukiukaji wa haki za binadamu utahitaji kushughulikiwa lakini akasisitiza kuwa hana uwezo wa kuliamuru jeshi la taifa hilo lenye ushawishi mkubwa.
Awali waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani, Rex Tillerson, alisema kuwa serikali ya Myanmar ni sharti ikome kuwahangaisha Waislamu wa kabila la Rohingya.

No comments:

Post a Comment