Ripoti za hivi punde kutoka nchini Uingereza zinasema kuwa mlipuko umetokea kwenye treni zinazokwenda chini kwa chini katika eneo la Kusini magharibi mwa mji mkuu wa London.
Abiria katika kituo cha wazi cha Parsons Green wamesema katika mitandao ya kijamii kwamba baadhi ya watu wamepata majeraha ya uso na kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa wakati watu walipokuwa wakijaribu kutoka katika treni hiyo.
Idara za kutoa huduma ya dharura zimewasili katika eneo hilo.
Picha zimeonyesha ndoo nyeupe ikichomeka ndani ya mfuko wa duka la jumla ,lakini mfuko huo hauonyeshi uharibifu mkubwa ndani ya treni hiyo.
Mashahidi wameelezea kuona abiria mmoja akiwa na majeraha ya uso.
Wengine wamesema kuwa kulikuwa na wasiwasi huku abiria wakitoka ndani ya treni hiyo katika kituo cha treni cha Parsons Green.
Huduma ya ambalensi inasema kuwa imetuma kikosi cha kukabiliana na majanga katika eneo hilo.
Mtangazaji wa BBC Riz Lateef aliyekuwa katika kituo hicho cha treni akielekea kazini alisema: kulikuwa na wasiwasi mwingi huku watu wakitoka ndani ya treni hiyo wakihofia maisha yao huku wakisema kulikuwa na mlipuko.
Wengi walipata majeraha ya kukatwa wakijaribu kutoroka eneo hilo.
Mwandishi wa BBC Sophie Raworth anasema kuwa alimuona mwanamke mmoja akiwa na majareha ya moto usoni na miguuni.
No comments:
Post a Comment