Mwandishi wa habari kutoka kaskazini mashariki mwa Nigeria ameshinda tuzo ya BBC la Komla Dumor.
Amina Yuguda ni mtangazaji katika kituo runinga cha eneo hilo cha Gotel, ambapo ameripoti kuhusu masuala kadha makuu ikiwemo kuhusu kundi la Boko Haram.
Yuguda atasafiri kwenda London kwa mafunzo ya miezi matatu mwezi Septemba.
Tuzo hili lilibuniwa kwa heshima ya Komla Dumor, mtangazaji wa runinga ya BBC ambaye alifariki ghafla akiwa na miaka 41 mwaka 2014.
Bi Yuguda amesema kuwa ushindi wake ni heshima kubwa.
Aliwavutia majaji kwa ripoti zake zinazohusu ushawishi wa radio nyumbani kwake.
"Kwa kisomo kidogo au kutokuwa na kisomo kabisa, wananchi wenzangu wanaelewa masula kadha ikiwemo uongozi wa Trump nchini Marekani, Korea Kaskania, Urusi chini ya Vladimir Putin na mengine mengi". Anasema Amina.
Mkurugenzi wa BBC World Service Group Francesca Unsworth, alisema Bi Yuguda alistahili ushindi huo.
Washindi wa awali wa tuzo la Kumla Dumor ni pamoja na mtangazaji raia wa Uganda Nancy Kacungira na mwandishi wa masuala ya biashara kutoka Nigeria Did Akinyelure
No comments:
Post a Comment