Wanandoa walio oana kwa miaka 75 wamefriki siku moja wakiachana kwa saa tano tu, ikiwa ni mwezi mmoja tangu washerekee ndoo yao wa miaka 75.
George mwanajeshi wa zamani na Jean Spear walikutana mwaka 1941 karibu na London wakati George akitoa huduma zake nchini Uingereza wakati wa vita vya pili vya dunia.
Wawili hao walifariki kwenye hospitali ya Ottawa siku ya Ijumaa baafa ya Bi Spear 94 kulazwa hospitalini.
- Wanawake Korea Kusini kuishi miaka mingi zaidi
- Watu walio na watoto huishi miaka mingi kuliko wale hawana
Alipewa tuzo la juu zaidi la Uingeza mnamo mwaka 2006.
Bi Spear na mumewa wa miaka 95 walikutana na Duke na Duches wa Cambridge wakati waliitembelea familia ya kifalme mwaka 2011.
Bw. Spear alilazwa katika hospitali ya Queensway Carleton siku ya Jumatano, siku moja baada ya mke wake kulwzwa, na kulala usingizi mkubwa.
Wahudumu wa hospitali walijaribu kumhamisha Bw Spear kwenda chumba alichokuwa mkewe, lakini Bi Spear akafariki alipokuwa akilala siku ya Ijumaa mwendo wa 04:30 kabla ya hilo kufanyika.
Bwana Spear naye alifarki muda mfupi baadaye mwindo wa saa 09:45.
Wameacha watoto wawili wakubwa Heather na Ian.
No comments:
Post a Comment