Thursday, September 21

Mtoto aliyehai agunduliwa kifusini

juhudi za uokoaji zikiendeleaHaki miliki ya pichaAUTHORITY
Image captionjuhudi za uokoaji zikiendelea
Waokoaji katika mji wa Mexico city wanajaribu kumfikia msichana mdogo, aliye hai chini ya kifusi cha jengo la shule, lililoporomoka wakati wa Tetemeko la ardhi lililotokea jana.
Wamekuwa wakimpitishia chakula na maji, wakati wakijaribu njia ya kuweza kumtoa salama kutoka katika maangamizi hayo.
Watoto wapatao 21 wamekufa baada ya jengo walilokuwamo kuvunjika, huku wengine wakiwa bado ndani ya kifusi hicho.
Wengine tetemeko liliwakuta wakiwa kanisaniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWengine tetemeko liliwakuta wakiwa kanisani
Jumla ya watu mia mbili na 25 wamefariki kutokana na tetemeko hilo.
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesema kila dakika imekuwa ikihesabika katika kuokoa maisha.
Tetemeko hilo la ardhi ni la pili kuipiga nchi hiyo mwezi huu.

No comments:

Post a Comment