Thursday, September 21

Rais wa Iran Hassan Rouhani aikosoa hotuba ya Trump kwa Umoja wa Mataifa

President Hassan Rouhani of Iran on screens at the UN General Assembly in New York, 20 SeptemberHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais wa Iran Hassan Rouhani aikosa hotuba ya Trump kwa Umoja wa Mataifa
Rais Hassan Rouhani wa Iran ametumia hotuba yake kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kumshambulia rais wa Marekani Donald Trump, kutokana na lawama alizotoa dhidi ya nchi yake.
Kwenye hotuba kwa Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, rais Trump aliijumuisha Iran kuwa kati ya mataifa maovu duniani.
Aliyataja makubaliano ya nyuklia kuwa aibu kwa Marekani.
Amesema kuwa nchi yake haitachukua hatua za kwanza kukiuka makubalaniano lakini akasema Iran itajibu hatua yoyote ya kukiuka makubaliano hayo.
An International Atomic Energy Agency (IAEA) inspector disconnects centrifuge cascades at the Natanz uranium enrichment facility (20 January 2014)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionIran inasema kuwa ina haki ya kuwa na nishati ya nyuklia na imesisitiza kuwa mpango wake ni wa amani.
Kitakuwa kitu kibaya ikiwa makubaliano hayo yataharibiwa na Bw. Trump.
Trump amekosoa makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa na Rais Barack Obama, mtangulizi wake.
Ikulu ya White House mwezi uliopita ilisema kuwa Iran ilikuwa inatimiza makubaliano hayo lakini Trump anasema kuwa Iran inayakiuka.
Mwaka 2015 Iran iliafikia makubaliano na mataifa mengi makubwa duniani yakiwemo Marekani, Uingereza, Ufaransa, China, Urusi na Ujerumani.
Arak heavy water nuclear facility (2011)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionIran inasema kuwa ina haki ya kuwa na nishati ya nyuklia na imesisitiza kuwa mpango wake ni wa amani.
Vikwazo vya kuharibu uchumi dhidi ya Iran viliondolewe na shirika la kudhibiti nyuklia duniani likasema kuwa Iran imepunguza shughuli zake za nyuklia.
Iran inasema kuwa ina haki ya kuwa na nishati ya nyuklia na imesisitiza kuwa mpango wake ni wa amani.
Men work inside a uranium conversion facility outside Isfahan (30 March 2005)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIran inasema kuwa ina haki ya kuwa na nishati ya nyuklia na imesisitiza kuwa mpango wake ni wa amani.

No comments:

Post a Comment