Korea Kusini imefanya mazoezi ya makombora yake kuashiria shambulizi dhidi ya Korea Kaskazini, kujibu jaribio la sita la nyuklia lililofanywa na Korea Kaskazini.
Mazoezi hayo yalihusu kurushwa kwa makombora ya masafa marefu kutoka kwa ndege za kivita na ardhini.
Hii ni baada ya waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis kuonya kuwa tisho lolote kwa Marekani au washirika wake kutoka Korea Kaskazini litajibiwa vikali kijeshi.
Korea Kaskazini ilisema kwa ilifanyia jaribio bomu la haidrojeni linaloweza kuwekwa kwa kombora la masafa marefu.
Korea mara kwa mara imekiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa na shinikzo za kimataiafa ya kuitaka iachane na mpango wake wa zana za nyuklia.
Ndani ya miezi mwili iliyopita, Korea Kaskazini imefanya majaribio ya makombra ya masafa marefu na hata kurusha kombora kupitia juu ya anga ya Japan hadi bahari ya Pacific.
Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wa dharura leo kujadili jibu la hatua hiyo ya Korea Kaskazini.
No comments:
Post a Comment