Serikali ya Venezuela imesema itachangia dola milioni tano kama msaada kwa wahanga wa kimbunga Hurricane Harvey kilichoipiga Texas mwishoni mwa mwezi uliopita.
Waziri wa mambo ya nje wa Venezuela Jorge Arreazza amesema msaada huo utatoka katika sehemu ya mapato ya kampuni kubwa ya mafuta ya Citgo.
Arreazza amesema kwa kuzingatia ubinaadam, nchi yake imeamua kuweka kando tofauti za kisiasa na kusaidia watu.
Citgo iliwekewa vikwazo vya kiuchumi mwezi uliopita kwa sababu kwamba Rais wa Venezuela Nicolas Maduro anakiuka haki za kibinaaman na kukandamiza demokrasia.
No comments:
Post a Comment