Monday, September 4

Kamera ya kupiga picha ndani ya mwili wa binadamu yagunduliwa

Kamera mpya inavyofanya kazi ya kubaini photons ndani ya mwili wa binadamuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKamera mpya inavyofanya kazi ya kubaini photons ndani ya mwili wa binadamu
Wanasayansi wamebuni kamera yenye uwezo ya kupiga picha viungo vya ndani ya mwili wa binadamu.
Kifaa hicho kimeundwa kuwasaidia madaktari kusaka vifaa vya madaktari, vinavyofahamika kama endoscopes, amvayo huenda vinaweza kusalia ndani ya viungo vya binadamu wakati wa upasuaji.
Hadi sasa, matabibu wamekuwa wakitegemea uchunguzi unaogharibu fedha nyingi, kama vile picha za X-ray, ili kufuatilia mafanikio yao.
Kamera hiyo mpya, itafanya kazi ya kubaini mwanzo wa mwangaza ndani ya mwili wa binadamu, kama vile sehemu ya ncha ya mwisho ya kifaa cha upasuaji cha tube ya endoscope.
Kifaa kihi kimeundwa kumsaidia madaktari kusaka vifaa vya kimatibabu vinavyojulikana kama endoscopes mwilini mwa binadamuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKifaa kihi kimeundwa kumsaidia madaktari kusaka vifaa vya kimatibabu vinavyojulikana kama endoscopes mwilini mwa binadamu
Profesa Kev Dhaliwal, wa Chuo Kikuu cha Edinburgh, anasema: "Ina uwezo mkubwa wa kutumika katika hali tofauti tofauti, kama vile inavyoelezwa ikiwa kazini. "Uwezo wa kuona iliko kifaa kilichosahaulika ndani ya mwili wa binadamu hasa katika sekta mbalimbali ya kitengo cha kiafya, huku tukisonga mbele kupunguza hali na mbinu ya kila aina ya kutibu maradhi mbalimbali."
'tishu na viungo'
Majaribio ya awali, inaonyesha kifaa cha prototype, kinaweza kubaini na kufuatilia mwangaza kupitia eneo la mshipa wa sentimita 20, katika hali tu ya kawaida.
Miali ya mwangaza kutoka kwa endoscope, inaweza kupenyeza ndani ya mwili, lakini mara nyingi hutawanyika au kuangazia nje ya mshipa na viungo, badala ya kupernyesa moja kwa moja mwilini.
Hali hii inatatiza hali ya kupata picha halisi ya iliko kifaa kilichoachwa mwilini.

No comments:

Post a Comment