Mwangosi amesema mwenyekiti wa chama hicho Dk Kyara anaumwa figo zote mbili tangu mwaka 2012 ambapo alienda nchini India mara mbili hivyo kwa sasa anafanyiwa matibabu ya kusafisha figo mara tatu katika hospitali ya Regency lakini bado ufumbuzi haujapatikana.
Amesema wakati anaendelea na matibabu hayo walimpata daktari mwenye mawasiliano na daktari wa hospitali ya Shijiazhuang, Dk Bryat ambaye alimtumia dawa ambazo zimeonyesha mafanikio ikiwemo kupata haja ndogo tofauti na awali alivyokuwa.
Mwangosi amesema kutokana na mafanikio hayo kuonekana hivyo amepewa rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali hiyo ambapo atatibiwa bila ya kuongezewa figo nyingine.
"Hadi sasa afya ya Kyara sio mbaya kama ilivyokuwa awali kwa sababu sasa anaendelea kutumia dawa za hospitali hiyo hivyo anahitajika akafanyiwe matibabu zaidi nchini China,"amesema.
No comments:
Post a Comment