Saturday, September 16

Askari wafungwa miaka 35


Mahakama Kuu imewahukumu kwenda jela miaka 35 wa kituo cha Polisi cha Osterbay jijini Dar es Salaam na watu wengine sita  baada ya kupatikana na hatia ya makosa  mawili ya ujangili.
Washtakiwa hao wamekutwa na hatia ya kupatikana na meno 70 ya tembo yenye thamani ya Sh 800 milioni na kujihusisha na mtandao wizi wa nyara za Serikali.
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Ama-Isaria Munisi baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka .
Washtakiwa waliotiwa hatiani na mahakama hiyo ni Ex Police D 8656 CPL Senga Nyembo,Ex Polisi G 553 PC Issa Mtama,Prosper Maleto, Seif Mdumuka, Amri Bakari, Said Mdumuka, Ramadhan Athuman,na Musa Mohamed.
Washtakiwa hao wamekutwa  na meno hayo katika eneo la kituo cha ukaguzi cha Kauzeni lililoko Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Katika kosa la kwanza washtakiwa wamehukumia kwenda jela miaka 20 kila mmoja na faini ya sh 8.5 bilioni kila mmoja wakati kosa la pili washtakiwa wawili ambao ni askari wamehukumiwa miaka 15 kwenda jela.
Pia Mahakama hiyo imeamuru gari lililokuwa limebeba meno ya Tembo kutaifishwa adhabu ambayo awali ilitolewa na Mahakama ya Kibaha mkoani Pwani.
Upande wa mashtaka uliwakilishwa na  Wakili Salimu Msemo akisaidia na Faraja Nchimbi.
Akizungumza kabla ya kutoa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Salimu Msemo  wameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa washtakiwa hao ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanapanga kujihusisha na ujangili wa nyara za serikali.
Wakati huohuo, Mahakama ya Wilaya ya Manyoni imemhukumu kwenda jela miaka 25 Saganda Kasanzu na kulipa faini ya sh 792 milioni kwa makosa ya kukutwa na nyara za Serikali pamoja na kujihusisha na mtandao wa nyara za Serikali.
Adhabu hiyo imetolewa na Hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo Joyce Minde baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na pande zote na kupelekea kutolewa kwa adhabu hiyo.
Mshtakiwa anadaiwa kukutwa na meno manne ya tembo yenye thamani ya Sh 66 milioni katika eneo la Kalangalasi lililop Wilaya ya Uyuwi mkoani Tabora.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Joyce amesema  kutokana na makosa hayo mshtakiwa huyo amehukumiwa kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kwanza na faini Sh660milioni kosa la pili amehukumiwa  kwenda jela miaka mitano na faini ya Sh 142 milioni

No comments:

Post a Comment