Hata hivyo ipo misemo ambayo ukiipa tafsiri ya neno kwa neno unajikuta unakwenda mchomo na kutoupata ujumbe uliokusudiwa.
Miongoni mwao ni ule msemo usemao kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kulala.
Ukiuangalia msemo huu juujuu utaona haingii akilini hata dogo kwa kelele katika chumba cha pili cha nyumba moja kisababishe usumbufu wa kumzuia mtu, awe mwenye nyumba au wapangaji wenzake kupata usingizi wa raha mustarehe.
Hata hivyo, si lengo langu hata kidogo kuzungumzia huo mkasa wa kelele za ndani ya nyumba za mpangaji ambazo tunaambiwa hazimzuii mwenye nyumba kulala, ninachokusudia kukieleza ni kukua kwa utamaduni mpya wa
kelele… kelele kelele kila pembe ya Zanzibar na wakati fulani hata ndani ya nyumba za ibada.
Kwa miaka mingi Zanzibar ilisifika kama visiwa shwari na watu wake kuwa wapole, makarimu na rahimu vyenye kiwango cha chini cha uhalifu.

Vitendo vya uhalifu vilivyofanyika Zanzibar hapo zamani ni kama vya kijana kuiba nguo zilizoanikwa kwenye kamba au watoto kulivuta kwa ndoana doriani lililopo kwenye meza ya duka.
Siku hizi hali ni tafauti kabisa. Unaposikiliza au kuangalia taarifa za habari katika radio na runinga za Visiwani au kusoma gazeti la serikali la Zanzibar Leo unaona habari nyingi za vitendo vya uhalifu, mauaji, ubakaji, matumizi ya dawa za kulevya na kadhalika vimetawala.
Lakini kama lipo jambo ambalo linakera na kusikitisha, lakini
linaonekana kufumbiwa macho na kutiliwa pamba masikioni ni kelele.
Karibu kila kila pembe ya Zanzibar utasikia kelele, kama vile watu wa
visiwa vya Unguja na Pemba hawaoni na ni viziwi au labda ndio
wameipokea kwa tafsiri potofu ule msemo wa “ Kelele za mpangaji
hazimzuii mwenye nyumba kulala.”.
Kwa mfano, katika soko kuu la mji wa Zanzibar kelele zimetia fora.
Hapa unakuta wafanya biashara wanaouza kanda za muziki, miutano ya
vyama vya siasa na mawaidha ya dini , wanaouza sumu ya panya na kwenye
maduka ya simu wakitangaza bidhaa wanazouza kwa kutumia vipaza sauti.
Ni kelele…kelele..kelele kla sehemu.
Gari za dala dala zimegeuzwa kumbi za muziki. Abiria hawawezi
kusikilizna na ukipigiwa simu bora usipokee kwa sababu hutaweza
kuwasiliana na aluyekupigia.
Vile vile matumizi ya ving’ora vya magari kwa misafara, hata ya magari
ya vikundi vya watalii yamekuwa mambo ya kawaida.
Lakini pia wapo abiria ambao wamekuwa wakiongeza kasi za kelele kwa
kufungua mzuziki za simu zao za mkononi kwa kelele kama vile
wamekodiwa kustarehesha abiriawaliopo safarini . Ni kawaida katika
dalala ukasikia kwa wakati mmoja hata nyimbo nne, ya taarab, Bongo
Fleva, Kiarabu na Kihindi kwa kwa wakai mmoja.
Mtu hatakosea akielezea safari kama hiyo ni ya watu ambao labda akili
zao zina matatizo.
Kinachosikitisha zaidi ni kuona hakuna sheria , kama zipo zimefumbiwa
macho na kuhifadhiwa ndani ya kabati, za kuidhibiti hali hii mbaya
na hakuna mtu anayekemea kama vile mambo haya ya kelele nyingi wakati
wote yanakubalika katika jamii ya kistaarabu.
.
Hu utamaduni wa kupenda kelele unaonekana hata katika maeneo ambayo
ukimya unahitajika sana, kama vile hospitali, misikitini na
makanisani.
Ni kawaida kuona wanaotembelea wagonjwa hospitali wanafanya zogo kwa
kuzungumza na simu zao za mkononi au wamevaa viatu vya visigino au
vile vyenye njumu na kusababisha kelele pale wanapopiga hatua katika
sakafu za wodi.
Hio miito mengine ya ya simu za mkononi kama ya Kuran na mengine ya
paka anayelia au mwana mama anayelilia mapenzi a nyimbo zenye ujumbe
ambao si mzuri kusikika hadhrani nayo inaongeza kelele na bughdha za
aina yake kwa
wagonjwa na wale wanaokwenda kuwajulia hali jamaa zao.
Jamii ya Wazanzibari inaoonekana kuupokea kwa mikono miwilina tabasamu
utamaduni huu wa kelele unaozusha fujo na kuathiri masikio na
kuhatarisha maisha ya watu.
Huko mitaani ndio mambo hayaelezeki. Kila mwenye radio au runinga
anaonekana kuwa na haki kufungua kwa sauti anayotaka radio au runinga
yake hata nyakai za usiku bila ya ujali huenda wapo watu waliola au
wagonjwa ambao wanahitaji hali ya utulivu.
Hata pale inapotokea kuwepo miba mtaani watu bado wanaona ni vizuri
kufurahia muziki wao bila ya kujali kwamba mila na tamaduni zinataka
uuone msiba wa jiani ni wako.
Katika baadhi ya vijiji, hasa vile katika fukwe wa pwani ambapo zipo
hoteli za kitalii na nyumba za agei na starehe, wana vjiji wamekuwa
wakilalamikia kelele kutok katika nymba hizi.
Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo kelele za wana vijiji za
kulalamikia kelele zimesikika na uchukuliwa hatua muwafaka, lakini
katika baadhi ya sehemu masikitiko yao hayazingatiwi kama vile
wanampigia gtaa mbuzi ambaye ni kiziwi.
Ni vizuri kwa viongozi wa serikali, jamii, mabaraza na halmashauri za
miji na wilaya kushirikiana na vyombo mbali mbali vya dola
kulitafakai suala hili kamakini na kulipatia ufumbuzi wa haraka
utakaoleta faraja.
Vyenginevyo, huu utamaduni wa kupenda na kuhabikia kelele ambao hivi
sasa umefikia kilele hapo baadaye utakuwa na athari mbaya zaidi kwa
watu wa Visiwani na kujkuta wanajjutia kwa kuvumilia kelele
zinazosikika hivi sasa..
Kama kelele za mpangaji hazimzuwii mwenye nyumba kulala ieleweke
kwamba kelele za vipaza sauti zinawakosesha watu usingizi na kuleta
bughudha yenye athari kwa mwili na akili za wana jamii.
Tujifunze kutoka nchi za wenzetu ambazo zimeweka sheria mbali mbali
zinazodhibti kelele za kipuuzi katika sehemu mbali mbali, ikiwa pamoja
na nyumba za starehe, kata vyombo vya usafiri na hata mitaani na
majumbani.
Tuachane na muhali na kuchukua hatua kuinusuru jamii na athari na
hatari zitokanazo na kelele.

No comments:
Post a Comment