Thursday, September 28

IGP Sirro awafariji askari walioathiriwa kwa moto


Arusha. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewasili eneo la nyumba za polisi zilizoteketekea kwa moto.
IGP Sirro amesema Rais John Magufuli ametoa Sh260 milioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi askari hao.
Amesema Jeshi la Polisi kupitia bajeti yake limetoa Sh40 milioni kwa ajili ya ujenzi huo.
IGP Sirro amesema jeshi hilo pia litatoa Sh1 milioni kwa kila familia iliyoathiriwa na moto huo. Katika nyumba zilizoteketea familia 14 zilikuwa zikiishi.
Kiongozi huyo wa Jeshi la Polisi amesema Rais Magufuli ameagiza Wakala wa Majengo (TBA) kutoa jengo la kuwahifadhi askari hao wakati ujenzi wa nyumba ukifanyika.
Amewataka wananchi wenye nia njema kuzisaidia kwa chochote walichonacho familia za waliounguliwa mali zao.
IGP Sirro na ujumbe wake ameelekea Tengeru kukagua jengo la TBA watakalotumia kwa muda askari hao.

No comments:

Post a Comment