Amesema hali hiyo ilitokana na suala la timing (la muda) kwa kuwa si vita kwamba useme Polisi walikuwa wamejipanga.
Mwigulu amesema matukio ya mauaji katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji yameligusa Jeshi la Polisi ambalo pia limepoteza askari wake.
“Mapambano na uhalifu ni suala endelevu. Hali ilivyo sasa ni tofauti, tunaendelea na mapambano na hatujui wao wanapanga nini,” amesema Mwigulu leo Alhamisi katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds.
Amesema, “Niwahakikishie wananchi usalama wa maisha yao na mali zao kwa kuendelea kupambana na uhalifu wa aina yoyote.”
Ili kukabiliana na wahalifu amesema Jeshi la Polisi limeanzisha Mkoa wa Kipolisi wa Rufiji, hivyo kuongeza ukaribu wa askari na masuala ya kiutawala na usimamizi.
Pia, amesema wameongeza vitendea kazi, doria na askari na kuboresha utafutaji wa taarifa za kihalifu ili kuwa mbele ya wahalifu.
No comments:
Post a Comment