Balozi Jensen amezungumza hayo mbele ya viongozi wa hospitali ya Marie Stopes iliyopo Mwenge wakati wa hafla ya ufunguzi wa hospitali hiyo ambayo imefanyiwa marekebisho.
Amesema Serikali ya Denmark kupitia Shirika la msaada la Denmark (Danida) itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto mbalimbali za jamii na uchumi.
"Tutaendelea kuwekeza kwenye sekta muhimu zaidi afya, elimu na vita dhidi ya umaskini. Lengo ni kuunga juhudi za serikali katika kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati," amesema Jensen.
Pia ameipongeza hospitali ya Marie Stopes kwa kuendelea kutoa huduma bora na za bei nafuu kwa wananchi ikiwemo huduma ya uzazi inayotolewa hospitalini hapo.
Balozi Jensen pia amezindua kitengo cha huduma kwa wateja kilichoanzishwa hospitalini hapo ambacho kinatoa fursa kwa wateja kupiga simu bure na kupata ufafanuzi kuhusu huduma zinazopatikana kwenye hospitali hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Marie Stopes nchini, Anil Tambay amesema marekebisho yaliyofanyika katika hospitali hiyo itaboresha utoaji wa huduma bora zaidi.
Hospitali ya Marie Stopes pia imeanzisha huduma ya upimaji bure wa magonjwa ya kansa, ukimwi ya siku tatu kuanzia leo mpaka Ijumaa mpaka Jumapili.
No comments:
Post a Comment