Wednesday, September 27

Chadema yamsimamisha katibu wake Moshi

Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil

Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema. 
Moshi. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kilimanjaro, kimezifuta barua walizoandikiwa madiwani sita wa Halmashauri ya Moshi, wakitakiwa kujieleza kwa usaliti.
Mbali na kufuta barua hizo zilizokuwa zimeandikwa na Katibu wa Chadema Wilaya ya Moshi, Emmanuel Mlaki chama hicho kimemsimamisha uongozi katibu huyo.
Madiwani hao akiwamo Mwenyekiti wa Halmashauri, Michael Kilawila walitakiwa kujieleza kwa madai ya usaliti kwa kumchagua makamu mwenyekiti wa halmashauri kutoka NCCR-Mageuzi.
Chadema na NCCR-Mageuzi ni vyama washirika katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), unajumuisha pia CUF na NLD.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema imesema barua zilizoandikwa na Mlaki ni batili na ameagiza ziondolewe katika rekodi za chama hicho.
“Tunautangazia pia umma kuwa Emmanuel Mlaki amesimamishwa uongozi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake na tunautaka umma kusitisha mawasiliano rasmi ya chama kupitia kwake.”

No comments:

Post a Comment