Wednesday, September 27

Mambosasa asema hajui miili iliyokutwa kwenye viroba imetoka wapi


Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema miili ya wanaume watatu iliyokutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach hawajui imetoka wapi hivyo wanaendelea na uchunguzi kubaini ilipotoka.
Mambosasa amesema jeshi la polisi linaendelea kupeleleza ili kujua miili hiyo imetokea mkoa upi, nchi gani na wajulikane watu hao ni wakina nani.
“Miili hiyo haieleweki inatoka wapi na watu wenyewe hawajulikani kama wanatoka Tanzania, Msumbiji au Angola hivyo tunaendelea kuichunguza,” amesema Mambosasa.
Maiti za watu ziliokotwa juzi katika eneo hilo mbili zilifungwa kwenye viroba huku nyingine imekutwa na jiwe kubwa lililofungwa na kamba.

No comments:

Post a Comment