Baadhi ya wabunge wapya nchini Kenya wamepinga mpango wa kupunguza mishahara yao kwa asilimia 15 kulingana na chapisho la mtandao wa Twitter wa chombo kimoja cha runinga.
Hatua ya kupunguza mshahara huo inayoshirikisha marupurupu kadhaa ilitarajiwa kuanza kutekelezwa baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti nane.
Mnamo mwezi Juni, tume ya marupurupu na mishahara ilisema kuwa mpango huo ulilenga kupunguza mishahara ya wafanyikazi wa serikali kwa asilimia 35.
Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wavunge wanaolipwa mishahara ya juu duniani, na hatua ya kuipunguza mishahara hiyo ni mojwapo ya mipango ya serikali kupunguza mishahara ya wafanyikazi wa serikali.
Mapato ya wastani nchini Kenya ni dola 150 kwa mwezi..
No comments:
Post a Comment