Thursday, August 24

Upigaji kura wakamilika Angola

Viongozi mbalimbali wakipiga kura
Image captionViongozi mbalimbali wakipiga kura
Zoezi la upigaji kura limekamilika nchini Angola ambapo inatarajiwa kuwa na Rais mpya baada ya José Eduardo Dos Santos kukaa madarakani kwa karibia miongo minne.
Baadhi ya sehemu za vijijini ambapo upigaji kura ulichelewa, ziliruhusiwa pia kuongeza muda wa kumaliza.
Kulikuwa na msisimko mkubwa wakati wa kampeni
Image captionKulikuwa na msisimko mkubwa wakati wa kampeni
Waziri wa zamani wa ulinzi João Lourenço anatarajiwa kushinda,lakini Dos Santos atasalia kama kiongozi mkuu wa chama cha MPLA.
Chama kikuu cha upinzani nchini Angola ni UNITA.

No comments:

Post a Comment