Thursday, August 24

Maduro atuhumiwa kuhusika katika rushwa Venezuela

Ortega alitoa shutuma hizo baada ya kukutana na waendesha mashtaka wa ukanda wa Amerika Kusini nchini Brazil
Image captionOrtega alitoa shutuma hizo baada ya kukutana na waendesha mashtaka wa ukanda wa Amerika Kusini nchini Brazil
Muendesha mamshitaka wa zamani wa Venezuela Luisa Ortega Diaz amesema kuwa ana ushahidi kwamba Rais Nicolous Maduro na kundi la maofisa wengine walipokea hongo kutoka kampuni moja ya ujenzi.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Brasilia, Ortega amewataja wanaotuhumiwa kuchukua hongo pamoja na Rais Maduro kuwa ni Makamu Rais chama tawala Diosdado Cabello na kiongozi mwingine wa chama Jorge Rodriguez.
Akizungumza kutoka mjini Caracas, muendesha mashitaka mpya Tarek Saab ambaye anatuhumiwa pia na Ortega anasema kuwa madai hayo yanakosa ushahidi.
Mbali na rushwa, Maduro anatuhumiwa kutumia nguvu zilizopitiliza dhidi ya wapinzani na raia
Image captionMbali na rushwa, Maduro anatuhumiwa kutumia nguvu zilizopitiliza dhidi ya wapinzani na raia
Amemkosoa Bi Ortega kwamba alifukuzwa utumishi serikalini kutokana na kufanya vitendo kinyume na maadili na kwamba ndani ya miaka kumi akiwa kazini ameshindwa kuchunguza tuhuma za rushwa.
Hata hivyo haya yanajiri, huku makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence akisema kuwa utawala wa Rais Trump unatarajia kuongeza nguvu dhidi ya Venenzuela ili kurejesha utawala wa kidemokrasia.
Pence anasema kuanguka kwa nchi ya Venenzuela kuna madhara kwa ukanda mzima na kusababisha ongezeko la usafirishaji wa dawa za kulevya na ongezeko la wahamiaji kinyume cha sheria.

No comments:

Post a Comment