Wednesday, August 30

Twaweza kuweka hadharani utendaji wa sekta ya afya leo

Sehemu ya matokeo ya utafiti wa Twaweza kuhusu

Sehemu ya matokeo ya utafiti wa Twaweza kuhusu sekta ya afya mwaka 2016 
Dar es Salaam. Baada ya kutoa ripoti ya utafiti wa hali ya usalama nchini mwezi uliopita, asasi ya kiraia ya Twaweza leo asubuhi inazindua matokeo ya utafiti mwingine unaoangazia changamoto za sekta ya afya.
Matokeo ya utafiti huo uliopewa jina la Sauti ya Wananchi, ulifanywa kati ya Mei 11 na 25 mwaka huu kwa kuhusisha sampuli ya watu 1,801 wa Tanzania Bara.
Miongoni mwa mambo yanayotazamiwa katika utafiti huo wa mfululizo wa 19 wa Sauti za Wananchi ni iwapo changamoto katika sekta ya afya zimepungua katika uongozi wa Serikali ya Rais John Magufuli, ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Twaweza inasema ripoti ya mwezi huu ambayo utafiti wake ulifanywa kwa njia ya simu inaweka bayana takwimu za mtazamo wa wananchi juu ya upatikanaji wa huduma za afya na ustawi wa jamii.
“Ni mambo gani wananchi hukutana nayo wakati wanaenda kupata huduma ya afya? Wanasubiri kwa muda gani kuzipata huduma hizo na je, hukumbana na uhaba wa dawa, watumishi au vifaa wanapoenda kutibiwa” inaeleza taarifa ya Twaweza kwa vyombo vya habari.
“Je, wanaotakiwa kupata huduma za bima wanazipata ipasavyo. Wananchi wangapi wana bima za afya? Ni wananchi wangapi wanafahamu huduma zinazotolewa na maofisa ustawi wa jamii wa wilaya?” inaongeza.
Mapema Agosti mwaka jana, Twaweza walizindua utafiti unaofa nana na huu ulioitwa “Nyota njema huuonekana asubuhi?” ambao pamoja na mambo mengine ulibainisha kuwa wananchi sita kati ya 10 hupata huduma za afya kutoka kwenye vituo vya afya vya umma.

No comments:

Post a Comment