Tuesday, August 22

Sumaye afunguka kuhusu mashamba yake


Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya

Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye 
Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amesema kunyang'anywa mashamba yake si sababu ya yeye kufikiria kurudi CCM.
“Kunyang’anywa mashamba yangu najua ni uamuzi wa juu haunidhoofishi nifikirie  kurudi CCM’’
Sumaye amesema mashamba yaliyofutwa na Serikali yalikuwa yanalipiwa kodi na yalikuwa yanamilikiwa kisheria.
"Wanataka nirudi CCM, mimi sitaki kurudi CCM, kwanini wananilazimisha?  Nilisema sababu za kuondoka huko, waseme wazi sababu za kuyafuta ni za kisiasa tu," amesema Sumaye leo katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment