Friday, August 11

Rais Magufuli awafurahisha wafanyakazi Tanesco


Dar es Salaam. Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco (Tuico) wamepongeza Rais John Magufuli kwa uamuzi wake wa kutekeleza mradi wa umeme wa maji Rufiji.
Akizungumza leo Alhamisi,Mwenyekiti wa Tuico Tanesco, Athuman Hassan amesema mradi huo wa megawati 2000 utakuwa na manufaa kwa uchumi wa viwanda.
"Wafanyakazi tunamuunga mkono, tutamsaidia kwa kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha tatizo la umeme Tanzania linakuwa historia,"amesema.
Amesema kukamilika kwa mradi huo wa Stieglers Gorge utamaliza tatizo la umeme na mwingine kuuzwa nje ya nchi.
Kuhusu vishoka, amesema watakuwa wakali kwa watu wanaojitambulisha kuwa ni wafanyakazi wa Tanesco wakati siyo.
"Tunaomba wananchi kutupa ushirikiano ili kuwatia nguvuni vishoka wanaowatapeli wateja wetu,"amesema.

No comments:

Post a Comment