Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amewasili nyumbani katika mji mkuu Abuja, baada ya likizo ya matibabu ya miezi mitatu mjini London.
Buhari amekuwa akiugua ugonjwa usiojulikana.
Wafuasi waliimba na kucheza densi walijipanga kwenye barabara za mji, ambapo maafisa wa ngazi za juu serikalini walikusanyika kumkaribisha Buhari.
Haijulikani ikiwa Buhari atarejea shughuli zke kamili kama rais.
Amefanya safari ya kupata matibabu London mara tatu tangu mwezi Juni mwaka uliopita.
Anatarajiwa kuhutubia taifa siku ya Jumatatu asubuhi. Kumekuwa na maandamano ya kumtaka Buhari arudi nyumbani au ajiuzulu.
No comments:
Post a Comment