Mwanamume mmoja nchini China alilipia sahani 5000 za chakula kwenye mji ulio kusini magharibi mwa nchi wa Chongqing, baada ya pete aliyokuwa ampe mpezi wake na iliyokuwa imepotea kupatikana.
Kulingana na gazeti Chongqing Morning Post, mwanamume huyo kwa jina Wang, alikuwa na nia ya kumshangaza mpenzi wake kwa kumuomba akubali kumuoa, baada ya kuchumbiana kwa mwaka mmoja.
Alikuwa amefanya maandalizi ya mpango huo lakini wakati alipokuwa akipata chakula cha mchana, ghafla aliondoka kwenye kiti chake kwenda kupokea simu.
Aliporudi alipata kuwa mkoba wake uliokuwa na pete ya almasi yenye thamani ya dola 44,900 ulikuwa umetoweka.
Lakini kwa bahati nzuri mfanyakazi mmoja wa mkahawa aliupata mkoba huo na kuukabidhi kwa meneja Yue Xiaohua ambaye baadaye aliurejesha kwa Bwana Wang
Bwana Yue aliambia gazeti la Chingqing Morning Post, kuwa bwana Wang alirudi kwenye mkahawa huo siku iliyofuata na kuuliza kuwa ni sahani ngapi za chakula walikuwa wanauza kwa siku.
Kisha akalipa jumla ya dola 5,200 sawa na sahani 5000 za chakula akisema kila mtu aalikwe ili apate chakula.
Gazeti hilo pia lilisema kuwa bwana Wang aliandika barua ya kushukuru mkahawa huo akisema kuwa mpenzi wake aliikubali pete hiyo.
No comments:
Post a Comment