Sunday, August 20

Grace Mugabe arudi Zimbabwe licha ya kutafutwa na polisi Afrika Kusini

Haijulikani ikiwa serikali ya Afrika Kusini ilimpa Bi Mugabe kinga ya kidiplomasia.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionHaijulikani ikiwa serikali ya Afrika Kusini ilimpa Bi Mugabe kinga ya kidiplomasia.
Vyombo vya habari nchini Zimbabwe zinasema mkewe rais Mugabe, Grace Mugabe amerejea nyumbani kutoka Afrika kusini licha ya kukabiliwa na mashtaka ya kushambulia mwanamitindo Gabriella Engels katika hoteli moja Johannesburg.
Inaeleweka kwamba Grace Mugabe alisafiri pamoja na mumewe leo asubuhi.
Wawili hao walikuwa wanahudhuria mkutano wa kikanda Afrika kusini.
Haijulikani ikiwa serikali ya Afrika Kusini ilimpa Bi Mugabe kinga ya kidiplomasia.
Mwamitindo Gabriella Engels 20, alimshtumu Bi Mugabe kwa kumpiga baada ya kumpata akiwa na watoto wake wawili wavulana ndani ya chumba kimoja cha hoteli huko Sandton, mtaa mmoja wa kifahari kaskazini mwa mji wa Johannesburg
Mwamitindo Gabriella EngelsHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMwamitindo Gabriella Engels
Bi Engels aliambia BBC kwamba alishambuliwa na bi Mugabe aliyeamini kwamba alikuwa akijua kule aliko mwanawe Bellarmine.
Mawakili wa Gabriella Engels mwanamke ambaye analaumu Bi Mugabe kwa kumgonga, wanasema kuwa mteja wao alipewa pesa kuachana na kesi hiyo lakini akakataa.
Bi Engels, alionekana kwenye mkutano wa waandishi waahabari siku ya Alhamisi akiwa na bendeji kubwa kwenye uso wake.
Grace Mugabe alikataa kufika mahakamani baada ya kushtakiwa wiki jana, akisema kwamba ana kinga ya kidiplomasia.
Mamalaka za Afrika kusini zimekanusha madai kwamba Grace Mugabe ana kinga ya kidiplomasia.

No comments:

Post a Comment