Tuesday, August 22

Panya wavamia na kuharibu afisi ya rais Buhari Nigeria

Rais Muhammadu BuhariHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRais Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammed Buhari atafanya kazi nyumbani kwa wiki tatu baada ya kurudi nchini humo kufuatia ziara ya matibabu nchini Uingereza.
Hii ni baada ya panya kuvamia na kuharibu afisi yake.
Msemaji wa rais aliambia BBC kwamba afisi ya Buhari inakarabatiwa baada ya panya kuharibu fanicha na kiyoyozi ndani ya afisi hiyo.
Aliongeza kuwa huku ikiwa bwana Buhari hawezi kufanya kazi katika afisi yake kutokana na hali ya afisi yake kwa sasa ,hatua yake ya kufanya kazi nyumbani haitaathiri kivyovyote utendakazi wake kwa njia yoyote.
Rais Buhari alirudi nchini Nigeria siku ya Jumamosi , baada ya kukaa mjini London kwa zaidi ya siku 100 ambapo alikuwa akipata matibabu.
Amekosolewa katika mitandao ya kijamii kwa kushindwa kuzungumzia kuhusu swala lake la afya katika hotuba kwa taifa siku ya jumatatu.
Hii ni baada ya panya kuvamia na kuharibu afisi yake.

No comments:

Post a Comment