Tuesday, August 22

Kiranja wa upinzani Tanzania Tundu Lissu akamatwa tena

Kiranja wa upinzani Tanzania Tundu Lissu akamatwa tena
Image captionKiranja wa upinzani Tanzania Tundu Lissu akamatwa tena
Mbunge kutoka chama cha upinzani Chadema, Tundu Lissu amekamatwa na polisi nje ya mahakama ya Kisutu iliyopo jijini Dar es Salaam na kupelekwa katika kituo kikuu cha polisi jijini humo.
Hii sio mara ya kwanza kwa Tundu Lissu kukamatwa.
Kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na kamatakamata hasa ya wanasiana kutoka upinzani.
Kulingana na gazeti la mwananchi nchini Tanzania wakili huyo alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili mfanyabiashara Yericko Nyerere mahakamani
Afisa wa idara ya Habari katika chama Chadema, Tumaini Makene amesema kuwa bwana Lissu alikamatwa na maafisa wa polisi alipokuwa akiondoka katika mahakama hiyo na kutakiwa kuelekea katika kituo cha polisi cha central

No comments:

Post a Comment