Hili ni kundi la pili kuachiwa kwa dhamana tangu walipotimiza masharti Julai 26, lakini wakaendelea kusota mahabusu ya gereza la Biharamulo mkoani Kagera kutokana na kukosekana kwa usafiri wa kuwafikisha mahakamani kukamilisha mchakato wa kuachiwa.
Kundi la kwanza la wana Chadema 14 liliachiwa Agosti 14 na hivyo kufanya waliopata dhamana kufikia 29 hadi jana.
Wanachama hao wamekuwa wakitoka kwa mafungu ambapo fungu la kwanza lilitoka Agosti 14 mwaka huu kwa viongozi na wananchma 14 kupewa dhamana ambapo jana wengine 15 wametoka na kufanya idadi yao kufikia 29.
Hakimu Mkazi Wilaya ya Chato, Jovith Kato amesema kuwa kundi lingine la watu 12 litaachiwa kwa dhamana kesho Agosti 23 huku, lile la mwisho la watu 10 likiwa ni keshokutwa
"Mahakama inalazimika kuwaachiwa kwa mafungu washtakiwa kutokana uwingi wao na mahitaji ya kupitia barua za wadhamini wawili kwa kila mshtakiwa," amesema
Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani Julai 10 na kunyimwa dhamana baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya zuio dhamana.
Hata hivyo, Hakimu Kato alitupilia mbali zuio hilo Julai 26, baada ya kukubaliana na hoja za wakili wa utetezi, Siwale Yisambi kuwa kifungu cha sheria kilichotumika kuzweka zuio hakikuwa sahihi.
No comments:
Post a Comment