Friday, August 25

DC Temeke awaonya wazoa taka



Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva 

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva  
Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amesema atawachukulia hatua za kisheria wazabuni waliopewa tenda ya kuzoa taka wanaotupa taka hizo eneo la Mwembe Yanga ikiwemo kulipa faini ya Sh1 milioni.
Lyavina aliyazungumza hayo baada ya kubaini kuwa wazabuni waliopewa tenda ya kuzoa taka wamekuwa wakitupa taka hizo eneo la Mwembe Yanga ambalo si rasmi kwa kutupa takataka hizo badala yake walitakiwa kuzipeleka Dampo la Pugu, Kinyamwezi.
 “Wale wote tuliowapa zabuni ya kuzoa taka wasiende kutupa takataka eneo la Mwembe Yanga, wanatakiwa kwenda kutupa kwenye Dampo la Pugu Kinyamwezi na atakayeshikwa atachukuliwa hatua ikiwemo kulipa faini ya Sh1 milioni,”alisema Lyaniva.
Pia alisema wananchi wajitokeze kufanya usafi kwenye maeneo yao ambapo mkuu huyo atashiriki kufanya usafi kwenye Kata ya Tandika.
Temeke bila uchafu inawezekana hivyo watendaji halmashauri hiyo wanatakiwa kusimamia usafi katika maeneo yao.
Diwani wa Kata ya Mtoni, Bernard Mwakyembe alisema wananchi wamekuwa wakitupa takataka pembezoni mwa barabara zikiwa kwenye mifuko ya plastiki jambo ambalo linaweza kusababisha milipuko ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Kipindupindu.
Suala la usafi ni lazima si hiari, kila mwananchi anatakiwa kufanya usafi kwenye eneo lake hivyo tunataka wilaya ya Temeke iwe mfano na ikiwezekana tuzishinde wilaya nyingine,”alisema Mwakyembe. 

No comments:

Post a Comment