Tuesday, July 25

Msigwa ammiminia sifa Wakili Fatma Karume



Wakili Fatma Karume

Wakili Fatma Karume 
Dar es Salaam. Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa, amesema Wakili Fatma Karume ni miongoni mwa watoto wa viongozi wanaojitambua.
Msigwa ameandika katika ukurasa wake wa instagram leo na kusema, Fatma anajitambua na ndiyo maana hatembelei jina la baba yake.
Fatma ambaye ni miongoni mwa washirika wa kampuni ya uwakili ya IMMA, ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
“Anajiamini, ni mshindani mzuri, ni mfano mzuri kwa wanawake hapa nchini,” amesema Msigwa.
Kwa sasa Fatma ndiye anamtetea Mbunge wa Chadema, Tundu Lissu katika kesi yake ya uchochezi.

No comments:

Post a Comment