Daktari huyo, Vejay Ramlakan aliongoza kikosi kilichomhudumia Mandela hadi kifo chake Desemba mwaka 2013.
Radio ya taifa nchini Msumbiji ilitangaza taarifa iliyotolewa na Machel ikilaani kitabu hicho vikali.
Machel amesema kuwa kitabu hicho kinakiuka heshima ya Mandela.
Kitabu hicho kimeandika taarifa kuhusu siku za mwisho kabla ya kifo cha Mandela, kimetaja kutokuwepo kwa maelewano kati ya madaktari na familia ya Mandela.
Machel anasema kuwa kitabu hicho kilikiuka siri iliyo kati ya daktari na mgonjwa.
No comments:
Post a Comment