Thursday, July 27

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA SKAUTI, AWAVISHA NISHANI VIONGOZI WASTAAFU


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa ufunguzi wa sherehe za miaka 100 ya Skauti Tanzania kwenye ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mlezi wa pili wa chama cha Skauti Tanzania kuanzia mwaka 1985 mpaka 1995 wakati wa sherehe za miaka 100 ya Skauti nchini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mlezi wa pili wa chama cha Skauti Tanzania kuanzia mwaka 2005 mpaka 2015 wakati wa sherehe za miaka 100 ya Skauti nchini zilizofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Bi. Fatma Karume kwa niaba ya Hayati Mhe. Abeid Amani Karume ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kuhimiza shughuli za Vijana wa skauti katika visiwa vya Unguja na Pemba kwenye  sherehe za miaka 100 ya Skauti nchini zilizofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Rais Mstaafu wa Awamu wa Sita wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume ambaye alikuwa mlezi wa pili wa chama cha Skauti Tanzania kuanzia mwaka 2000 mpaka 2010 wakati wa sherehe za miaka 100 ya Skauti nchini zilizofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim ambaye alikuwa skauti tangia shuleni na alipokuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika ambapo mwaka 2001 alipendekeza kuwe na siku ya SKAUTI AFRIKA itakayokuwa inaadhimishwa kila tarehe 13 mwezi Machi. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments:

Post a Comment