Saturday, July 29

Kim atamba kupata uwezo wa kuipiga Marekani



 Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanya majaribio ya kombora lake la masafa marefu (ICBM) lenye uwezo wa kupiga bara lolote na kwamba jaribio hilo onyo kali kwa Marekani.
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amesema baada ya jaribio hilo sasa wana uwezo wa kupiga eneo lolote na kuifuta Marekani katika uso wa dunia kwa sababu kombora hilo lina uwezo wa kufika katika mji wowote.
Jaribio la kombora hilo limefanyika wiki tatu baada ya jaribio la kombora la kwanza la masafa marefu.
Rais wa Marekani, Donald Trump, amelitaja jaribio hilo kuwa la kijinga na kitendo cha hatari kilichotekelezwa na utawala wa Korea Kaskazini.
China pia imeshutumu jaribio hilo huku ikitaka pande husika zilizo na wasiwasi kujizuia ili kutoendeleza wasiwasi zaidi.

No comments:

Post a Comment