Rais wa Marekani Donald Trump amemteua Waziri wa Usalama wa Ndani, John Kelly kuwa mkuu wa shughuli za Ikulu ya White House baada ya kumfuta kazi Reince Priebus.
Priebus, aliyetumikia wadhifa huo kwa miezi sita, ameondolewa baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuhusu hatima yake na Trump alitangaza uamuzi wake kwenye mtandao wa Twitter alipowasili mjini Washington akitokea New York.
Trump alimmwagia sifa Kelly kwa kazi anayofanya katika wizara. Imeelezwa kwamba sababu kubwa ya kumfuta kazi Priebus ni madai kwamba alikuwa kiongozi dhaifu.
Mapema wiki hii mkurugenzi mkuu mpya wa mawasiliano wa Ikulu ya White House Anthony Scaramucci, alimtuhumu hadharani Preibus kuhusiana na uvujaji wa habari za kumharibia sifa Rais Trump kwenye vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment