Mtwara. Serikali imetakiwa kukaa na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Aliko Dangote kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokikabili kiwanda hicho kwa kuwa anaweza kuwa balozi wa wawekezaji nchini.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe ametoa ombi hilo jana akisema Dangote ana jina kubwa, iwapo kungekuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji angesaidia kuwavutia wengine.
“Siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kadhaa katika vyombo mbalimbali vya habari zinazohusiana na kiwanda cha Dangote, kutozalisha kwa kile kinachoelezwa ni kutokana na hitilafu za ufundi. Kwa kuwa tatizo la ufundi limejitokeza kipindi ambacho tayari kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wamiliki juu ya gharama za uzalishaji, inasababisha kuwapo mkanganyiko kujua kiini cha tatizo,” amesema Akwilombe.

No comments:
Post a Comment