Monday, October 9

Makerere yapoteza kiongozi muhimu katika safu yake

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda na naibu mwenyekiti wa Mamlaka ya Mipango ya Taifa, marehemu Dr Abel Rwendeire atapewa heshima zote za kiserikali wakati wa maziko yake Jumapili.
Wakati wa ibada maalum iliyofanyika katika eneo la Kumbukumbu ya Mashujaa huko Namugongo Ijumaa, Waziri Mkuu Dr Rwendeire aligusia kuwa Dr Rwendeire atazikwa kiserikali Jumapili katika mji wa wazee wake huko Kibuzigye, Wilaya ya Rubanda.
“Hivi sasa bunge liko mapumzikoni, lakini mara litapoanza shughuli zake kutakuwa na mswada wa kuruhusu waheshimiwa Wabunge kutoa heshima zao kwa Dr Rwendeire,” alieleza.
Waziri Mkuu ambaye alikuwa amefuatana na Naibu Waziri Mkuu wa pili Kirunda Kivejinja na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali, alitoa maombolezo juu ya waziri mkuu huyo aliyeaga dunia na kusema kuwa “ni mwanasayansi adimu sana, mwanasiasa, kiongozi na mwanazuoni.
Marcy Rwendeire, mjane wa marehemu, alimuelezea mumewe kama ni mtu mwenye upendo na kuahidi kuchukua jukumu la kuwasimamia na kuwatunza watoto wao sita.
“Mume wangu aliaga dunia ghafla. Tulikuwa tumekaa tunaangalia televisheni pale aliponiambia kuwa anahisi maumivu kwenye kifua yanaongezeka,” alieleza, na kuongeza kuwa ilikuwa wakati wa asubuhi wakati alipogundua kuwa mumewe hawezi kuongea.
Majirani zetu walitusaidia kumpeleka hospitali lakini tulipofika tukaambiwa tayari ameaga dunia,” amesema.
Mkewe amesema kuwa alikutana naye mwaka 1978 Chuo Kikuu cha Makerere na walikuwa washerehekee miaka 40 ya ndoa yao mwaka 2018.
Mary Kobusingye Oyuru ambaye alizungumza kwa niaba ya watoto wa marehemu alisema baba yao alikuwa “ni mfano wa kuigwa na wengine.”
“Alitufundisha mambo mengi na kutupa elimu bora kabisa na hivyo kutuwezesha sote kupata shahada za juu,” alieleza.

IEBC yataka Mahakama ya Juu ifafanue marejeo ya uchaguzi


Majaji wa Mahakama ya Juu Kenya.
Mahakama ya Juu nchini Kenya itatoa maelekezo Jumatatu katika kesi iliyofunguliwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IECB ambayo inataka ufafanuzi ni jinsi gani ikabiliane na mapungufu iwapo yatajitokeza katika uhakiki wa matokeo ya uchaguzi wa marudio.
Vyama vyote vilifahamishwa Ijumaa kuwa vinatakiwa kufika mahakamani Jumatatu ilikupata muongozo vipi masuala ya uchaguzi yatavyokuwa.
Kupitia kwa wakili Kamau Karori, Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ameitaka mahakama kutoa ufafanuzi tume ifanye nini kukabiliana na makosa yatakayo jitokeza baada ya uhakiki wa fomu za matokeo ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa Karori, kuna mkangamano juu ya uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo Septemba 20, kwa sababu majaji walinang’ania kuwa mwenyekiti ni lazima ahakiki matokeo kabla ya kutangaza mshindi wa kinyang’anyiro cha urais.
Amesema ni muhimu kwa mahakama kutoa ufafanuzi iwapo Chebukati na Tume yake wanaweza kusahihisha makosa ya Fomu namba 34B, wakati matokeo yatapokuwa hayalingani na yale yaliyosajiliwa katika Fomu namba 34A.
Walipofikiwa Jumamosi kuulizwa kuhusu suala hilo, wakili wa Muungano wa upinzani wa NASA Jackson Awele amesema kuwa walikuwa wamepokea nyaraka za mahakama Alhamisi na bado hawajawasilisha maelezo yao mahakamani.
“Bado tunalifanyia kazi suala hili,” alisema.
Mahakama ya Juu, kwa uamuzi wa walio wengi, ilibatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais Agosti 8 ikitaja kuwa ulikuwa umegubikwa na dosari nyingi na kukiuka katiba wakati wa kupeperusha matokeo hayo.
Jaji Mkuu David Maraga, Makamu wake Philomena Mwilu, Majaji Smokin Wanjala na Isaac Lenaola walitoa uamuzi kuwa dosari na uvunjifu wa sheria ulikuwa mkubwa kiasi cha kuathiri matokeo.
Majaji Jackton Ojwang’ na Njoki Ndung’u hawakukubaliana na uamuzi huo.

Marekani yasitisha huduma ya kutoa visa kwa Uturuki

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani.
Ubalozi wa Marekani huko Ankara nchini Uturuki umeeleza kwamba Marekani imesitisha kwa muda maombi yote ya visa za wasiotaka uhamiaji kutoka uturuki.
Taarifa ya ubalozi Jumapili inaeleza kwamba kufuatia matukio ya karibuni yalilazimisha serikali ya Marekani kutathmini tena dhamira ya dhati ya serikali ya Uturuki kwa usalama wa ofisi zake za ubalozi na wafanyakazi. Taarifa haikuelezea sababu zinazopelekea kutathmini tena dhamira ya uturuki wala haikusema usitishaji huo wa utoaji visa utadumu kwa muda gani.
Mfano wa Visa ya Marekani
Mfano wa Visa ya Marekani
Hata hivyo taarifa iliongeza ili kupunguza idadi ya wageni kwenda ubalozi wetu na ubalozi mdogo wakati tathmini inaendelea kuanzia sasa wamesitisha kwa muda huduma zote za visa za wasio taka kibali cha uhamiaji kwenye ubalozi wetu mdogo huko Uturuki.
Saa kadhaa baadae Uturuki nayo ilijibu kwa kutangaza usitishaji wake wa huduma za visa 

Rais Trump atangaza matakwa yake ya mabadiliko ya sheria za uhamiaji

Rais Donald Trump wa Marekani
Rais wa Marekani Donald Trump aliweka wazi Jumapili kwamba ili kufikia makubaliano na wademocrat kuruhusu wale wahamiaji wanaofahamika kama 'Dreamers' kuendelea kukaa Marekani, atashinikiza kurekebisha mfumo kamili wa kibali cha ukaazi maarufu kama 'Green Card' akitaka kuajiri maafisa wa uhamiaji zaidi ya 10,000 na kujenga ukuta kwenye mpaka wa kusini.
Mwezi uliopita Rais Trump alitangaza mpango wa kufutilia mbali mradi wa Deferred Action for Childhood Arrivals-DACA, sera ya enzi ya utawala wa rais wa zamani Barack Obama ambayo inawalinda maelfu ya vijana ambao waliingia nchini kama watoto kinyume cha sharia.
Sera ya uhamiaji ya Rais Trump inajumuisha kupunguza kuwapatia wake na watoto wa mtu mwenye kibali cha ukaazi halali yaani Green Card au kwa raia wa Marekani, na badala yake kubuni mfumo wa kutoa natija kwa ajili ya jamaa hao. Lakini wademocrat mara moja wamepinga vikali matakwa hayo ya rais.

Kapteni raia wa Iran ameuwawa katika maji ya Somalia


Meli za uvuvi katika maji ya Somalia.
Maafisa wa jimbo la Puntland huko Somalia walisema kapteni mmoja wa boti ya uvuvi raia wa Iran aliuwawa na pia baharia mwingine alijeruhiwa baada ya wanajeshi wa usalama kufyatua risasi wakati wa operesheni katika bahari ya Hindi.
Maafisa walisema ufyatuaji risasi ulitokea baada ya maafisa wa polisi wa ulinzi wa bahari wa Puntland kuona boti mbili zilizoshukiwa zinavua kinyume cha sheria siku ya Ijumaa katika bahari ya Somalia. Kanali Mohamed Abdi Hashi wa polisi Puntland aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba boti hizo mbili zilipuuza amri ya kusimama na zilijaribu kukimbia.
Alisema wanajeshi wao wa usalama walikua wanafanya operesheni hapo Oktoba 6 ndipo walipokabiliana na boti mbili za uvuvi haramu kwenye pwani ya Ras Hafun. Wakati walipojaribu kuwasimamisha kwa ajili ya kuangalia kibali chao cha uvuvi walikimbia .
Kanali Hashi alisema wakati wa ufyatuaji risasi ndipo Haydar Abdalla Sabiul wa boti ya Al-Sa’idi aliuwawa na baharia wa pili alijeruhiwa na watu 16 wengine hawakujeruhiwa lakini walikamatwa.

ARUSHA WAANZA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAANZA KWA KISHINDO

Wananchi wa Kata za Themi, Sekei na Sombetini Wilaya ya Arusha mjini leo wameanza zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa kishindo; huku baadhi wakihangaika huku na huko kutoa nakala ya viambatisho vyao ili kujisajili kwa wakati.

Akizungumza katika Usajili huo Afisa Usajili wa Wilaya hiyo Bi. Juliet amesema wamepanga kukamilisha usajili wa Kata hizo ndani ya siku 9; na kwamba wananchi wote wanaoishi katika Kata hizo kujitokeza kwa wingi ili wasajiliwe.

Misururu ya wananchi imeonekana katika Kata za Themi na Sekei; huku baadhi wakihangaika kujaza fomu za maombi ya Usajili. Katika hali iliyoonyesha ushirikiano na kujizatiti kwa viongozi katika kuhakikisha wananchi hao wanahudumiwa, ofisi za Mitaa leo zilifungwa kwa muda na huduma zote kuhamia katika makao makuu ya Kata ili kuwaidhinishia wananchi fomu zao pamoja na kuwagongea mihuri kuthibitisha makazi yao.

Zoezi la Usajili kwa Wilaya ya Arusha Mjini linatazamiwa kukamilika ndani ya miezi miwili; ambapo wananchi wataweza kupata namba za Utambulisho (NIN) wakati hatua za uzalishaji Vitambulisho zikiendelea. Wilaya nyingine mkoani humo ambazo usajili unaendelea ni Karatu, Longido, Arumeru na Monduli.
Mmoja wa Wageni Wakaazi mkoani Arusha na mkazi wa Kata ya Sekei akikamilisha Usajili wa Vitambulisho vya Taifa. Zoezi la Usajili kwa mkoa wa Arusha linahusisha wananchi wenye umri wa miaka 18 na kuendelea na Wageni Wakaazi wenye kuishi halali nchini.
Watumishi wa NIDA wakiingiza taarifa za wananchi kwenye mfumo kutumia mashine maalumu ya Usajili ambayo pia inauwezo wa kuhifadhi si tu taarifa za kawaida pia alama za kibaiolojia na picha za waombaji wa Vitambulisho wakati wa Usajili.
Ofisi ya Kata ya Themi ambako zoezi la Usajili limeanza rasmi, na kukutanisha mamia ya wananchi kupata huduma.

Afisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Uhamiaji makao makuu Arusha akihakiki uraia wa mmoja wa wananchi katika Kata ya Themi aliyefika kujiandikisha.

BENKI YA CRDB YACHANGIA UJENZI WA VYOO WILAYANI CHATO

Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus, akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi vifaa hivyo katika halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita.

Walioketi ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodluck Nkini, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji CRDB.

Na Binagi Media Group.
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, benki ya CRDB imechangia vifaa vya ujenzi wa vyoo katika shule za halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita ili kusaidia utatuzi upungufu wa vyoo katika shule za halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus alisema vifaa hivyo vitasaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi za Kalema, Muungano na Katemwa A na kwamba vifaa hivyo vimejumuisha mifuko 150 ya theruji, mabati, sinki za vyoo pamoja na vyombo vya kukusanyia taka na tenki la maji kwa ajili ya halmashauri ya Chato.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas aliishukuru benki hiyo na kubainisha kwamba bado kuna uhaba wa vyoo kwenye shule nyingi na kuiomba kuendelea kusaidia utatuzi wa changamoto hiyo ili kutoa chachu kwa wadau na benki nyingine kuiga mfano huo.

Zoezi la kukabidhi vifaa hivyo lilifanya ijumaa Oktoba 06,2017 katika halmashauri ya wilaya ya Chato ikiwa ni muda mfupi baada ya benki ya CRDB kutoa semina kwa wateja wake wilayani humo na pia kutoka maeneo jirani ikiwemo Muleba, Katoro na Biharamulo.
Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga, akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi vifaa hivyo.
Zoezi la kukabidhi vifaa vya ujenzi wa vyoo katika shule za halmashauri ya Chato.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wakipokea vifaa hivyo.

SHUHUDIA MTI WENYE UMRI WA MIAKA 500


SABA WANUSURIKA KIFO BAADA YA GARI WALIYOPANDA KUGONGA TRENI JIJINI TANGA

Watu saba wamenusurika kifo huku wawili  wakijeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo baada ya gari ndogo waliokuwa wamepanda aina ya Carry kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni ya Tanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda, gari hilo baada ya kufika eneo la makutano ya reli wakati likijaribu kusimama  lilifeli breki na kuiparamia treni hiyo.
Ajali hiyo ambayo ilitokea jana eneo la makutano ya reli Kwaminchi Jijini  Tanga iliacha mshangao mkubwa kutokana na mazingira ya namna ilivyotoke ambapo gari ndogo ilikuwa ikitokea eneo la Kwaminchi.
Akithibitisha kutokea tukio hilo jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba alisema ajali hiyo ilitokea saa kumi jioni katika eneo hilo ambapo gari hilo ilifeli breki na kuparamia mabehewa ya reli wakati ikipita katika eneo hilo.
Aliitaja gari hiyo aina ya Carry ambayo ilipata ajali hiyo kuwa ni T.343 DCQ  iliacha njia na kuigonga treli iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuingia  kwenye stesheni ya Tanga.
Aidha alisema majeruhi sana waliokuwepo kwenye ajali hiyo walifikishwa  kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kwa matibabu zaidi huku Dereva wa gari hilo akitokomea.
Kamanda huyo alisema kutokana na kukimbia kwa dereva huyo wataendelea kumsaka ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kamanda huyo alitoa wito kwa madereva kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani kwa kuhakikisha kwenye maeneo ya kivuko cha reli wanakaa mita 50.

 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga
 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba akikagua gari hiyo jioni hii. 

WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WAMETAKIWA KUSIMAMIA WELEDI KATIKA KAZI ZAO


 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaban akizungumza wakati wa mahafali ya 8 ya  Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi katika Sherehe ya Mahafali ya nane ya bodi  yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
 Wahitimu wa Shahada ya Ununuzi na Ugavi  wakiwa katika Maandamano  wa Mahafali ya nane ya bodi ya watalaamu wa ununuzi na Ugavi.

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaban akiongoza Maandamano wakati wa mahafali ya 8 ya  bodi ya Watalaamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika  Moshi(MOCU), Neema Kumburu  akipokea cheti cha chuo hicho kuongoza katika utoaji wa masomo hayo mwaka wa pili Mfululizo
 Hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi akitoa nasaha kabla ya kumkaribisha mgeni Ramsi katika Mahafali ya 8 ya chuo hicho
 Wahitimu wa Shahada ya Utaalamu wa Ununuzi na  Ugavi (PSPTB) wakisoma Kiapo Mbele ya Mgeni Rasmiwakati wa mahafali ya 8 ya  bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi,Ahmed Kilima akitoa hotuba ya Shukrani wakati wa kufunga  mahafali ya 8 ya  bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Wahitimu wa Shahada ya Utaalamu wa Ununuzi na  Ugavi (PSPTB),  katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 8 ya bodi

Wafanyakazi wa bodi ya Ununuzi na ugavi wakiwa katika picha ya pamoja na  mgeni rasmi na meza kuu wakati wa kuhitimisha Mahafali ya 8 ya bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi

Brass Bendi kutoka Jeshi la Magereza nchini wakitoa Burudani wakati wa Mahafali ya Nane ya Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi

MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KATIKA ZIARA YA THAILAND

Na Richard Mwaikenda
Akizungumza mjini Dar es Salaam wakati wa kikao cha maandalizi na baadhi ya Wana Mkikita watakaokwenda Thailand, Mtaribu wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Resorce Afrika Limited, Idrissa Songoro amesema kuwa maandalizi ya ziara hiyo kwa upande wa Thailand kwa asilimia kubwa yako tayari.
Amesema kuwa ziara hiyo ya wiki moja Wanamkikita watanufaika kwa mambo mengi, ambapo licha ya kutangaza vivutia mbalimbali vya utalii pia wataonesha utamaduni wa mapishi ya kila aina ya vyakula vya asili vya Kitanzania.
Amesema Wanamkikita ambao miongoni mwao ni Wakulima, Wafanyabiashara na Wajasiriamali watapata wasaa wa kubadilishana mawazo na wenzao wa Thailand kwa lengo la kukuza ushirikiano katika masuala ya kibiashara,kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa.
Songoro amewaasa Wanamkikita kufanya maandalizi  ya uhakika ili wakienda Thailand wanufaike na ziara hiyo na kuwa na mrejesho mzuri watakaporejea nyumbani.


"Kitabia Wathailand wanafanana na Watanzania, kwani ni wakalimu, wapole, waungwana lakini pia ni wachapakazi na wako makini sana katika kila jambo wanalolifanya,"amesema Songoro.



Amesema kuwa Ujumbe huo utapata pia fursa ya kutembelea eneo la viwanda, mashamba ya wakulima pamoja na eneo la utafiti wa kilimo la Chiang Mai na Mji Mkuu wa Bangkok.



"Wathailand wana elimu mkubwa katika nyanja ya uhifadhi wa vyakula na kuviongezea thamani pamoja na kutangaza logo za kibiashara,. Pia wana mbegu za mazao mbalimbali zinazotoa mazao mengi kwa hekali, kwa mfano unaweza kuzalisha kabeji tani 25 kwa heka moja,"amesema Songoro.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kisui S. Kisui  aliwaasa Wanamkikita kuichangamkia ziara hiyo kwani watakaokwenda watanufaika kwa kupata fursa mbalimbali za maendeleo ikiwemo masuala ya kilimo cha kisasa na biashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo, Adam Ngamange alielezea jinsi Mkikita ilivyopanga kuwaandaa wanajachama watakao kwenda huko kwa kuwapiga msasa kwa kutumia vikao na semina mbalimbali ili wawe na uelewa kwa kujua mambo mbalimbali watakayokwenda kufanya katika ziara hiyo muhimu.
Aliimpongeza Songoro kwa jitihada zake kwa kujitolea kwa moyo mkunjufu kuratibu ziara hiyo itakayokuwa na makubwa kwa Mkikita, Wanachama na Tanzania kwa ujumla.
 Mtaribu wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Resorce Afrika Limited, Idrissa Songoro akizungumza kuhusu maandalizi ya ziara ya mafunzo ya Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA),nchi Thailand inayotarajia kuanza katilati ya mwezi ujao Novemba mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo, Adam Ngamange na Mwenyeikiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kisui . Kisui.UJUMBE wa Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) unaokwenda ziara ya mafunzo nchini Thailand, umejiandaa pia  kwenda kuutangaza utalii wa Tanzania.
 Songoro na viongozi wa Mkikita wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanamkikita wanaotarajia kwenda Thailand kwa ziara ya wiki moja.
 Dk. Kisui akielezea jinsi Mkikita ulivyojipanga kwa ziara hiyo, itakayowanufaisha wanachama kwa kukutana ana kwa anakwa mazungmzo  na wafanyabiashara na wakulima wa Thailand pamoja na kuingia nao mikataba mbalimbali. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Ngamange akifafanua jambo kwa wajumbe
 Ngamange akiwa na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mkikita wakati wa kikao hicho 
 Baadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao wakimsikiliza Songoro


 Songoro akifafanua jambo katika kikao hicho
 Ngamange akitoa shukrani kwa Songoro kwa uratibu wa ziara hiyo pamoja na kukubali kushiriki kwenye kikao hicho

 Elizabeth Ndangoba Mkurugenzi wa Fedha na Utawalawa Mkikita
 Catherine Edward Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mkikita
 Adam Ngamange
 Dk. Kisui akisisitiza jambo alipokuwa akifunga kikao hicho
 Songoro akijadiliana mambo na wajumbe wa Mkikita
 Mjasiriamali Mwambapa akiwa na Ngamange
 Songoro akihojiwa na African Swahili Televisheni
 Ngamange, Rose na Dk Kisui
Songoro akiwa na Mwambapa pamoja na Ngamange.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
-KAMANDA WA MATUKIO BLOG

IGP SIRRO AWASILI MKOANI SONGWE KWA ZIARA YA KIKAZI


 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, alipowasili mkoa humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia pamoja na kuwakumbusha wajibu wa kutoa huduma bora kwa jamii. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili katika mkoa wa Songwe, kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia pamoja na kuwakumbusha wajibu wa kutoa huduma bora kwa jamii. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo na kupeana mbinu na mikakati namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu ikiwamo upitishaji wa magendo kutoka nchi jirani unaofanywa na watu wasiowema. IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi. 
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, wakiwa katika picha na  Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, baada ya kumaliza kikao kazi cha kupeana mbinu na mikakati namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu ikiwamo upitishaji wa magendo kutoka nchi jirani unaofanywa na watu wasiowema. IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.