Monday, October 9

Kapteni raia wa Iran ameuwawa katika maji ya Somalia


Meli za uvuvi katika maji ya Somalia.
Maafisa wa jimbo la Puntland huko Somalia walisema kapteni mmoja wa boti ya uvuvi raia wa Iran aliuwawa na pia baharia mwingine alijeruhiwa baada ya wanajeshi wa usalama kufyatua risasi wakati wa operesheni katika bahari ya Hindi.
Maafisa walisema ufyatuaji risasi ulitokea baada ya maafisa wa polisi wa ulinzi wa bahari wa Puntland kuona boti mbili zilizoshukiwa zinavua kinyume cha sheria siku ya Ijumaa katika bahari ya Somalia. Kanali Mohamed Abdi Hashi wa polisi Puntland aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba boti hizo mbili zilipuuza amri ya kusimama na zilijaribu kukimbia.
Alisema wanajeshi wao wa usalama walikua wanafanya operesheni hapo Oktoba 6 ndipo walipokabiliana na boti mbili za uvuvi haramu kwenye pwani ya Ras Hafun. Wakati walipojaribu kuwasimamisha kwa ajili ya kuangalia kibali chao cha uvuvi walikimbia .
Kanali Hashi alisema wakati wa ufyatuaji risasi ndipo Haydar Abdalla Sabiul wa boti ya Al-Sa’idi aliuwawa na baharia wa pili alijeruhiwa na watu 16 wengine hawakujeruhiwa lakini walikamatwa.

No comments:

Post a Comment