Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya wanawake wa chama cha Mapinduzi (UWT) Sophia Simba amewataka wanawake kuandaa kushika nyadhifa mbalimbali kwa kujitokeza kugombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025.
Sophia Simba amesema hayo leo alipokuwa akihutubia Kongamano la Wanawake wa UWT lenye lengo la kuenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo yametimiza miaka 60.
" katika kuyaenzi Mapinduzi Matukufu kama wanawake ambao tulishiriki moja kwa moja ni wakati Wetu sasa nasi kuchukua nafasi za Uongozi katika Majimbo, Kata na Mitaa" amesema Sophia Simba.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda amemshukuru Mama Sophia Simba kwa kukubali mwaliko huo na kuweza kuvuka mpaka visiwani humo kwa ajilinya kutoa neno kwa wanawake ambao ni Nguzo ya Chama cha Mapinduzi.
Mama Chatanda aliendelea kushukuru kwa kusema UWT imara ya leo ni matokeo mazuri ya Malezi yake mazuri kwa wanawake akiwa Mwenyekiti.
"Nakumbuka nilitoka kwenye mikono yake na kunipa Baraka za kwenda kugombea jimbo la Korogwe na Hatimae nikafanikiwa kuwagaragaza wanaume hivyo alinitia moyo na kuniambia kuwa naweza " Amesema Mama Chatanda.
Aliongeza kuwa na hata alivyosikia nimechukua fomu ya kugombea uenyekiti wa UWT Taifa aliiinuka na kunisemea vyema kila mahala kwa kutamka kuwa huu ni wakati sahii wa Maria kushika hii nafasi.
Kwa Upande wake Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa na Mwenyekiti wa Zanzibar Mama Zainabu Shomari aliendelea kwa kuwashukuru wajumbe na Watoa mada kwa kuweza kufika katika kongamano
Mwenyekiti Mstaafu wa UWT Taifa, Sophia Simba akizungumza na wanawake wa Jumuiya Visiwani Zanzibar katika Kongamano Maalum la kuhadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Taifa Mary Chatanda, akizungumza na wanawake wa Jumuiya ya wanawake wa Visiwani Zanzibar katika kongamano la kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa, Bi Zainabu Shamari akitoa neno kwa wajumbe.
Katibu Mkuu wa UWT, Jokate Mwegelo akizungumza na wanawake wa Jumuiya hiyo wa Visiwani Zanzibar katika Kongamano Maalum la kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment