Leo ni siku ya malaria duniani. Tafiti bado zinaonyesha kuwa dunia inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo maambukizo , udhibiti na tiba, hasa katika bara la Afrika.
Takwimu kutoka shirika la afya duniani (WHO), zinaonyesha maambukizo million 216 ya malaria na vifo 445,000 vilivyotokana na malaria mwaka 2016, duniani.
Kati ya asillimia 90 ya wanaouguwa malaria na asilimia 91 ya vifo hivyo vilitokea barani Afrika.
Katika eneo la Afrika Mashariki , japo idadi ya vifo vinavyotokana na malaria vimepungua bado raia wa mataifa hayo wako hatarini kukumbwa na maambukikzo mapya.
Nchini Tanzania asilimia 93 ya raia wako hatarini , huku kenya ikiwa na aslimia 70 ya idadi ya watu walioko hatarini kupata malaria.
Llicha ya juhudi mbali mbali kuelekezwa katika kuzuia ugonjwa huo, bado mataifa hayo ya Afrika Mashariki yanakabiliwa na changamoto kutokomeza mbali ugonjwa huo.
Ripoti ya WHO inaeleza kuwa kina mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5 bado wako hatarini zaidi.
Siku hii inajiri wiki moja baada ya makongamano mawili ya malaria ikiwa ni kongamano la 7 la wanasayansi barani Afrika nchini Senegal na lile la kimataifa lililoandaliwa pembeni ya mkutano wa nchi za Jumuiya ya Madola jijini London nchini Uingereza.
Marais pamoja na viongozi wakuu serikalini, wanasayansi na wadau wengine wa afya duniani walikusanyika kutathimini mbinu mpya za kutokomeza ugonjwa huo, jijini London.
Akihutubia kwenye kongamano hilo rais uhuru Kenyatta alisema kuwa juhudi za kupunguza maambukizi mapya zimefanikiwa ambapo afrika mashariki idadi ya maambukizi mapya yamepungua kutoka asilimi 11 hadi 8.
Matibabu bila malipo na upatikanaji wa dawa za kutibu malaria ni kati ya juhudi zilizochangia kupunguza vifo kutokana na malaria.
Tangia mwaka 2011 vyandarua vya kujikinga na mbu vilisambazwa kwa kila mtu katika maeneo yaliyo athiriwa na malaria Afrika kwa ushirikiano wa serikali na mashirika yasiyo ya serikali.
Takwimu zikionesha kuwa zaidi ya vyandarua vya kuzuia mbu milioni 15 vimesambazwa kwa wakenya katika kaunti 23 zilizo katika hatari ya kuambukizwa malaria. Hata hivyo matumizi ya vyandarua hivyo yangali changamoto.
Shirika la Malaria No More, ni kati ya mashirika ambayo yanaendeleza kampeni ya kupiga vita ugonjwa huo hasa nchini kenya.
Ripoti ya shirika hilo ikionyesha kuwa japo juhudi zaidi zinahitajika , tathimini yao imedhihirisha kuwa Wakenya wanajikinga na kutafuta huduma za afya kwa wakati.
Julie Chege ni msimamizi wa shirika hilo nchini Kenya anasema: "Katika juhudi za kuzuia maambukizi ya malaria, shirika la afya ulimwenguni limetangaza kuwa kwa mara ya kwanza chanjo ya kwanza duniani kukinga malaria itaanzishwa katika maeneo ya Ghana, Kenya na Malawi baadae mwaka huu."
Kenya ikiwa miongoni mwa watakaopata huduma hizo za chanjo, Chege akariri kuwa wanatarajia huduma hizo hivi karibuni.
Maadhimisho ya siku ya malaria duniani yameshuhudiwa katika mataifa yaliyoathirika na malaria kama njia ya kuhamasisha raia kuhusu mbinu za kujikinga na ugonjwa huo hatari.
No comments:
Post a Comment