Saturday, April 28

Chaguo la Trump wizara ya wanajeshi wastaafu ajiondoa

Daktari Ronny Jackson
Daktari wa White House, mwenye cheo cha Rear Admiral Ronny Jackson, amejiondoa Alhamisi katika nafasi aliyopendekezwa na Rais Trump ya kuongoza wizara inayo hudumia wanajeshi wastaafu wakati wabunge wakiendelea kuchunguza madai kuwa alikiuka maadili na kujihusisha na ulevi wa kupindukia.
Wakati akijitoa katika uteuzi huo, Jackson alieleza kuwa kitendo cha kumshutumu ni “madai ya uongo,” lakini amesema shutuma hizo “zimekuwa kizuizi” dhidi ya juhudi za Rais Donald Trump katika kuboresha huduma ya afya kwa wanajeshi wastaafu wa Marekani
Trump katika mahojiano na kipindi chake anachokipendelea zaidi cha mazungumzo ya habari, “Fox & Friends,” aliendelea kumtetea Jackson, ambaye ni daktari wake binafsi, akisema, “ Shughuli anazofanya zinavutia.”
Trump amemlaumu Seneta Jon Tester, Mdemokrat kutoka Montana, kwa kuuwa uteuzi wa Jackson katika nafasi ya baraza la mawaziri kusimamia idara inayoshughulikia wanajeshi wastaafu milioni 13 na ina wafanya kazi 377,000.
Tester amesema Jumatano kuwa hivi sasa wafanyakazi 20 na wanajeshi wa zamani ambao wanaifahamu ofisi ya Jackson waliwaambia wabunge kuwa alikuwa na tabia ya kunywa pombe ofisini, na usimamizi wake ulikuwa na hali ya mvutano na alikuwa akitoa dawa bila ya kuchunguza historia ya mgonjwa.
“Wanajaribu kumuangamiza mtu,” Trump amesema. Hakuna ushahidi juu ya shutuma hizi.” Amesema Tester “lazima atalipa thamani kubwa” kisiasa juu ya maoni yake dhidi ya Jackson.

Kiongozi huyo wa Marekani amesema hivi sasa “anaye mtu fulani ambaye anauzoefu wa kisiasa,” katika fikra zake ambaye atampendekeza kuchukua nafasi ya Jackson ili aweze kuongoza wizara hiyo.

No comments:

Post a Comment