Wednesday, April 4

Waziri Hamad ahimiza wanawake kujitokeza chanjo ya saratani



Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed
Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed 
Zanzibar. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imewataka wanawake kujitokeza kupatiwa chanjo, ili kujikinga na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.
Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed alitoa wito huo wakati akizindua mkutano wa uhamasishaji uliowahusisha wakuu wa wilaya na mikoa.
Alisema saratani ya kizazi ni hatari zaidi hivyo wanawake wanatakiwa kujitokeza kupata kinga ambayo inatolewa bure.
Hamad alisema takwimu zinaonyesha aina hiyo ya saratani inayoongoza Tanzania, ikiwamo Zanzibar kwani wanawake 51 kati ya 100,000 wanaathirika na ugonjwa huo.
Pia, alisema wanawake 38 kati ya 100,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa huo na inakadiriwa wastani wa wanawake 466,000 wanagundulika kuwa na saratani hiyo kila mwaka kwa nchi zinazoendelea.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo walisema upo umuhimu wa kusambaza elimu waliyoipata.

No comments:

Post a Comment