Isaac ni kijana mwenye umri wa miaka 15,ambaye alishuhudia kundi la wanaume wakimkamata kwa nguvu msichana mdogo.
Ilikuwa mkesha wa kuamkia mwaka mpya katika mtaa wa Kibera,eneo ambalo lina idadi kubwa ya wakazi wanaoishi maisha duni nchini Kenya na hali hiyo ilimfanya ajue kuwa dada huyo alikuwa katika matatizo.
Na pia alijua kuwa hana nguvu ya kupambana na wanaume hao ambao walikuwa wakubwa kwake.Alikuwa amefundishwa kutoingilia kati ugomvi wa namna hiyo,hivyo Issac aliamua kwenda kumuita mwanaume mwingine ili aweze kumsaidia binti yule.
"Kila mtu alianza kulalamika" ,Isaac alieleza.Wanaume wale walisema lazima wambake.
Baada ya dakika ishirini,waliamua kumuachia.
Ukisikiliza simulizi za aina hii zinashangaza sana ,alisema Anthony Njangiru mratibu wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Ujamaa,ambayo inawafundisha wavulana kama Isaac kuzuia unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake katika makazi duni ya mji mkuu wa Kenya,Nairobi.
Sio kila mtu ana bahati,alisema.
Kubadili tabia
Bwana Njangiru anafundisha kipindi kinachoitwa "Your Moment of Truth to boys"(Ni muda wako wa ukweli) unaolenga vijana wa kiume wenye umri wa miaka 14 mpaka 18 katika shule za sekondari.
Yeye ni miongoni mwa wakufunzi wengi, na darasa hilo linafundisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na elimu ya mahusiano,changamoto za imani potofu juu ya ubakaji,makubaliano na namna ambavyo wanaweza kuingilia kati kama vijana hao wakishuhudia unyanyasaji huo.
Programu ya "sources of Strength" inayohusu mabadiliko ya mwili imewalenga vijana wa umri wa miaka 10 mpaka 13.
Programu hiyo ina mafunzo ya muda wa masaa mawili kwa wiki.Kila darasa limegawanyika mara mbili katika wiki sita,likiwa na wasichana ambao kila mmoja amefundishwa mbinu zake.
Tangu taasisi hiyo ya Ujamaa ianzishwe,imewafundisha watoto zaidi ya laki mbili na nusu katika shule zaidi ya mia tatu mjini Nairobi.
Mafunzo hayo ambayo yamelenga kubadili mtazamo wa wavulana dhidi ya wasichana
"Kama sisi wavulana na wanaume ni sehemu ya matatizo basi tunaweza kuwa sehemu ya suluhisho",bwana Njangiru alisema.Tunaweza kuwa watu wa kwanza kubadilika.
Wakubali wanapokataliwa
Programu hii pia imewafundisha wavulana kuacha kuwa na fikra za kudhani kwamba msichana akisema "hapana" kwa tendo la ngono basi anakuwa anamaanisha "ndio".Au kuona ni sawa kwa msichana kubakwa kwa sababu tu amevaa nguo fupi.
Wanajaribu kutumia udhaifu wa wasichana ili kujinufaisha wenyewe,alisema bwana Njangiru,"kama atasema hapana lakini kwao hiyo kukataliwa inaeleweka tofauti na wanaenda kufanya watakavyo wao.
Unyanyasaji dhidi ya wanawake
Unyanyasaji wa kingono umekuwa ni tatizo la kidunia na programu kama hizi nchini Kenya,zinawafundisha vijana namna ya kubaini unyanyasaji wa kingono na namna ya kukabiliana nao.
Kiwango cha unyanyasaji kwa wanawake nchini Kenya ni kikubwa.
Hali hii ni mbaya zaidi pale utakapoingia katika mitaa ya wakazi wa hali ya chini,ambapo tafiti zimeeleza kuwa wasichana zaidi ya robo wa eneo hilo wamenyanyaswa kingono mwaka jana
Mafunzo haya yanayotolewa na Ujamaa yalibuniwa chini ya programu ijulikanayo kama "No means No wordwide" katika jitihada zake za kupunguza unyanyasaji wa kingono katika mji mkuu wa Kenya.
Mwaka 2010,walianza kwa kuwafundisha wasichana waliopo shuleni mjini Nairobi namna ya kukataa na namna ya kubaini tatizo na kuongelea njia ambayo wanaweza kupambana nao
Kama "hapana" inadharauliwa ,basi wanapaswa kujifunza mbinu za kukabiliana nao na kulenga kupiga sehemu muhimu kama za macho na magoti.
Kujisimamia
Mapendekezo ya tafiti yanasema matatizo mengi yanakuja kutoka kwa marafiki wa kiume.
Hivyo 'Ujamaa' ikaamua kuongeza wigo zaidi kwa kuwajumuisha wavulana katika mafunzo hayo ,
bwana Njangiru alisema,hii inatokana na mwenendo wa wavulana kuwa na mchango mkubwa wa unyanyasaji wa kingono.
Barani Afrika,wanaume wamekulia katika mazingira ambayo yanawafanya waamini kuwa wanawake hawana lolote la kusema na wanaume ndio hupewa kipaumbele,hivyo tunataka kubadili kwanza huo mtazamo.
Asasi hii inawapa motisha vijana wa kiume kuwa na moyo zaidi wa kutokomeza unyanyasaji kuendelea kwa kutumia mbinu mbali mbali.
Tunawataka vijana wa kiume kuwa na ujasiri wa kusimamia kile wanachokiamini kuwa hakipo sawa,bwana Njangiru aliongeza.
Lakini kila siku tunawakumbusha kuhusu usalama wao .Hawapaswi kuumia kama wataingilia katika tukio fulani.
Kama maisha yao yako hatarini,wanapaswa kuwajulisha wenzao au utawala.
Kufanya jambo lililo sahihi
Programu hii ya Kenya imeweza kufanikiwa na sasa imeanzishwa Malawi na kuna mpango wa programu hiyo kuanza Uganda.
No comments:
Post a Comment