Akizungumza waandishi wa habari leo Aprili ofisini kwake Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Dk, Faustine Ndugulile amesema kuwa vituo hivyo vimefungwa kufuatia opreresheni maalum iliyofanywa Machii mwaka huu katika mikoa 11 ya Tanzania Bara.
Amesema katika operesheni hiyo wamegundua kuwa kuna baadhi ya wataalam wa tiba asili ambao wanatumia vifaa ambavyo havijasajiliwa kwenye utoaji wa tiba mbadala kama vile mashine za utra sound, upimaji wa Virus vya ukimwi, Malaria, Kisukari na shinikizo la Moyo (Pressure),
huduma ambazo zimekuwa zikitolewa bila ya kuwa na wataalam wa magonjwa hayo.
Operesheni hiyo ilifanyika katika mikoa 11 ambayo ni Dar es Salaam, Morogoro, Singida, Arusha, Kilimanjaro Mbeya, Rukwa, Kigoma, Mwanza, Kagera na Mtwara kwa muda wa siku mbili kuanzia Machi 6 hadi 7 mwaka huu.
“Idadi ya vituo vilivyofungiwa ni pamoja na mkoa wa Dar es Salaam tumevifungia vituo 16, Singida vituo vitatu, Arusha vituo saba, Mbeya vituo 11, Rukwa vituo vinne, Kigoma kituo kimoja, Mwanza vituo vitatu,Kagera vituo viwili na Mtwara vitu vitatu, ambapo kwa mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro hakuna vituo tulivyovifungia,” amesema Dk, Ndugulile.
Kwa upande wake Dk, Ruth Suza, msajili wa Baraza la tiba asili kutoka Wizara ya afya alisema kuwa zoezi la kukagua na kuvifungia vituo vya tiba asili ambavyo havina sifa ni endelevu ili kila mmoja aweze kutoa
tiba sahihi kutokana na taaluma yake.
Amesema kwa mikoa iliyobakia watafanya ukaguzi pia ili kuhakikisha kuwa huduma zote zinazotolewa na wataalam wa tiba asili na tiba mbadala ni zile tu ambazo zinastahili kutolewa na wataalamu hao na si
vinginevyo.
Naye Mkurugenzi wa dawa na Vifaa vya nyongeza kutoka Wizara ya afya, Dk, Adam Fimbo amesema kuwa ukaguzi huo hautahusisha wataalam waliosajiliwa tuu bali na wale ambao hawajasajiliwa ili kuhakikisha kuwa kila mtaalam wa tiba asili anatoa huduma inayokubalika kutokana
na utaalamu wake.
“Operesheni hii inafuatia uwepo wa taarifa za uwepo wa matumizi ya vifaa tiba aina ya magnetic quantum analyzer na vingine vinavyofanana na hivyokwenye vituo vya tina asili na tiba mbadala kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa na matangazo ya vifaa hivyo yanayopotosha umma,” amesema dk Fimbo
No comments:
Post a Comment