Jumba la makumbusho la Victoria na Albert lililoko nchini Uingereza limetoa pendekezo la kurudisha kwa mkopo mali za Ethiopia zilizonyakuliwa na wanajeshi wa Uingereza miaka 150 iliyopita, ikiwa ni pamoja na taji la dhahabu, vazi la harusi la kifalme na kikombe cha divai cha dhahabu.
Pendekezo hilo lilitolewa baada ya vitu kadhaa kufikishwa kwenye maonyesho hadi mwezi Juni 2019 katika jumba hilo la maonyesho mjini London ili kuadhimisha vita vilivyotokea Maqdala mwaka 1868.
Wanahistoria wanasema ndovu 15 na nyumbu 200 walihitajika kubeba mali yote iliyoibiwa kutoka eneo la Maqdala, mfalme mkuu Tewodros II kutoka makao makuu yake kaskazini mwa nchi hiyo.
Ethiopia waliwasilisha ombi mwaka 2008 kwa taasisi tofauti za Uingereza la kurudisha mali hizo zenye thamani ya mamilioni ya dola zilizochukuliwa kutoka Maqdala.
Mkurugenzi mkuu wa V&A Tristram Hunt amesema kwamba bidhaa hizo zitasalia kuwa mali ya jumba hilo la maonyesho lakini zitarudishwa nyumbani kwa ''mkopo wa muda mrefu''.
Maqdala 1868
- Katikati mwa karne ya 19 mfalme mkuu Tewodros aliamua kuiboresha hekalu lake kwa muundo wa kisasa , Abyssinia, kwa kufungua uhusiano na Uingereza.
- Lakini mambo yalizidi kutumbukia nyongo baada ya ombi la kutaka usaidizi wa kijeshi ulipotupiliwa mbali.
- Kama njia ya kupinga hilo, mfalme mkuu akamkamata mwanabalozi wa Uingereza na wageni wengine kutoka nchi za nje.
- Uingereza walijibu kisa hicho kwa kutuma jeshi lake kwenye ngome ya mwanamfalme huko Maqdal
- Licha ya kuwa mfungwa, mwanamfalme Tewodros alijitoa uhai wake.
- Wanajeshi wa Uingereza waliwachiwa na nyaraka , misalaba, vikombe vya dhahabu vya divai ,ishara za dini , nguo za kifalme zinazotumika kanisani , ngao na silaha.
- Mtoto wa mwanamfalme mwenye umri wa miaka saba pia alichukuliwa na Uingereza na alipokea mafunzo katika shule ya raga:
- Alifariki kutoka na ugonjwa wa kufura kwa mapafu akiwa na miaka 18 na akazikwa katika kasri ya Windsor- serikali ya Ethiopia imeomba pia masalio ya kijana huyo kurudishwa.
- Benki kuu ya Uingereza iliwekeza taji la dhahabu na kikombe cha dhahabu cha divai katika jumba la V&A mwaka 1872.
- Na bidhaa nyengine za V&A zinazohusiana na Maqdala zililetwa baadaye kama msaada wa kibinafsi na ununuzi.
Bw Hunt aliambia gazeti la The Art kwamba pendekezo hilo liliwasilishwa kwa balozi katika ubalozi wa Ethiopia mjini London , lililoipatia ushauri jumba la V&A wakati wanapojitayarisha kwa maonyesho yanayotarajiwa kufunguliwa siku ya Alhamisi.
Jumba la V&A limesema vitu 20 ambavyo vinatarajiwa kupelekwa kwenye maonyesho vitawaruhusu watazamaji wapya kufahamu uzuri kwa bidhaa zao kwa mifano na utaalam mkubwa kwa ushonaji wa nguo na utengenezaji wa chuma ili kutafakari kwa kina historia ya vitu hivyo.
Maonyesho hayo yatakuwa na mifano ya hapo awali ya picha za silaha zilizotumika na wanajeshi nchini Uingereza ambazo jumba hilo limesema ni miongoni mwa picha za kwanza kabisa kupigwa na wanajeshi wa Uingereza, kabla ya teknolojia kamili ya sasa ya kupiga picha kuboreshwa.
Baadhi ya vitu vilivyokuwa vimeshikiliwa na mataifa ya Ulaya na vimerudishwa Afrika
Tanzania : Barakoa ya Makonde, iliwasili Musée Barbier-Mueller, Geneva , na mwaka 1985 ilirudishwa nchiniTanzania tarehe 10 mwaka 2010.
Afrika Kusini: masalio ya Saartjie Baartman (Hottente Venus), yalichukuliwa kwenye kijiji kimoja kilichoko Afrika Kusini mwaka 1810. Lakini jumba la maonyesho la Musée de l'Homme, Paris uliurudisha mwaka 1994.
Angola: Sanamu ya ''Lwena'' kutoka ilitwaliwa na polisi wa Ufaransa katika mnada uliofanyika Saint-Germain-en-Laye, tarehe 24 mwezi Machi mwaka 1996 na kurudishwa nchini Angola mnamo 28 Oktoba, 1997.
Mali: Sanamu ya kondoo aliyokabidhiwa Jacques Chirac mwaka 1991, aliyekuwa ametwaliwa kutoka kwa wachimbuaji wa vitu vya kale nchini Mali ilirejeshwa nchini humo Januari 1998.
No comments:
Post a Comment