Shirika la Uingereza linalofuatilia usawa katika jamii, Tume ya Usawa na Haki za Kibinadamu, limetoa wito wa"hatua za dharura kuchukuliwa'' ili kuwalinda wahasiriwa na visa vya unyanyasaji wa kingono kazini.
Hapa wanawake sita vijana wanasimulia mifano sita ya jinsi wanawake husumbuliwa kazini.
Maelezo na Emma Russell.
Ushuhuda huu umetolewa na Tume ya Usawa na Haki za Kibinadamu na Wakfu wa Wanawake Vijana.
"Kisa kibaya zaidi -mteja akija kazini anajipendekeza -iliniacha nikiwa na uoga sana.
Tangu hapo nimekuwa makini sana na nguo ninazozivaa,sketi zinazopanda juu ninapoketina mikufu ya kuning'inia, na kadhalika''
''Nilikuwa na miaka 17. Ilibidi nijifungie chooni kutokana na matamshi ya mzaha yaliyobadilika kuwa tishio, wahudumu wenye umri mkubwa walikuwa wakisema mzaha kwamba nani angenivunja ubikira wangu kwa sababu nilikuwa nimpenda kwenda kanisani."
''Nilikuwa nikifanya kazi kwenye tamasha moja ya upigaji wa picha na mwanamume mmoja akanishika kutoka nyuma Kwa hivi sasa najiepusha kuvalia sketi fupi. Tunastahili kuweka wazi kwamba unyanyasaji wowote unaweza kumfuta mtu kazi''
''Nilifanya kazi kwenye kilabu na mteja mmoja alinisukuma kwenye ukuta na akajaribu kuweka mikono yake kwenye suruali yangu ya ndani -kwenye kilabu kilichojaa watu, sehemu ambayo kila mtu angeweza kuniona''
''Kitu kibaya zaidi nilisalia pekee yangu na sikuwa na mtu wa kumtegemea bali nilipatwa na mshtuko kila mara kwa wiki nzima, kulia wakati ninapolala, kupata msongo wa mawazo kuhusu vitu vidogo na kunisababishia kupata matamanio ya kula kila mara."
''Nilimfahamisha mkubwa wangu afisini kuhusu unyanyasaji lakini viongozi wa kampuni hiyo walikuwa wanaume walidhani naongeza chumvi. Wanawake wengine watano waliacha kazi kutokana na unyanyasaji wa kingono uliosababishwa na mwanamume mmoja kwa kipindi cha mwaka mmoja.''
Ushuhuda huu umetolewa na kamati ya pamoja ya Tume ya Usawa na Haki za Kibinadamu na Wakfu wa Wanawake Vijana.
No comments:
Post a Comment