Saturday, April 28

Sokwe mzee zaidi kwenye hifadhi afariki Marekani

Colo alifariki akiwa na umri wa miaka 60 na kuushi miaka mingi zaidi kuliko sokwe wengineHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionColo alifariki akiwa na umri wa miaka 60 na kuushi miaka mingi zaidi kuliko sokwe wengine
Sokwe anayefahamika kuwa mzee zaidi na ambaye ni wa kike kwa jina Colo, ameaga dunia nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 60.
Colo aliaga dunia akiwa amelala katika hifadhi ya Columbus kwenye jimbo la Ohio chini ya mwezi mmoja baaada ya kusherehekea siku ya kuzaliwa.
Alizaliwa kwenye hifadhi hiyo mwezi Disemba mwaka 1956, na inaaminiwa kuwa sokwe wa kwanza kuzaliwa akiwa kwenye hifadhi.
Hofadhi ya Columbus katika taarifa, ilisema kuwa Colo alikuwa ni balozi wa sokwe wengine, aliyewafunza watu kuhusu familia hiyo ya wanyama iliyo kwenye hatari ya kuangamia.
Sokwe Colo akifurahia keki yake
"Colo alibadili mawazo ya watu wengi ambao walifika kumuona pamoja na wale waliomuhudumia katika maisha yake," taarifa hiyo ilisema.
Hifadhi hiyo ilisema kuwa maiti yake itachomwa na majivu kuziwa eneo hilo.
Mwezi Disemba mamia ya watu walitembelea hifadhi ya Columbus kumuimbia Colo wimbo wa kuzaliwa na kumtazama akifurahia keki yake.

No comments:

Post a Comment