Friday, April 6

Shoo ya Werrason Dar yasogezwa mbele


Dar es Salaam. Shoo ya mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Werrason Ngiama iliyokuwa ifanyike leo Ijumaa Aprili 6, 2018 kwenye ukumbi wa Escape One imeahirishwa kutokana na mwanamuziki huyo kuchelewa kufika nchini.
Kuchelewa huko kumetokana na hati za kusafiria za Werrason na wanamuziki wake nchini DRC kuchelewa, hivyo kukwamisha taratibu nyingine za kusafiri.
Taarifa za kuahirishwa kwa shoo hiyo zimetolewa leo na Katibu Mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (Chamudata), Hassan Msumari.
“Kundi  hili litaingia nchini Tanzania kesho Jumamosi na wote waliokata tiketi za onyesho la Escape One wazitunze kwa ajili ya kuzitumia tarehe itakayotangazwa la kundi zima la Wenge Mason Mere linaingia Jumamosi,” amesema Msumari.
Werrason ni miongoni mwa vijana waliojiunga pamoja mwanzoni mwa miaka ya 1980 na kuanzisha bendi ya Wenge Musica BCBG wakishirikiana na JB Mpiana, Didier Masela na Alan Makaba.

No comments:

Post a Comment