Tuesday, April 10

Mkuu wa zamani wa majeshi Sudan Kusini aunda vugu vugu jipya la waasi

Raia wa Sudan ya KusiniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRaia wa Sudan ya kusini
Aliyekuwa Mkuu Majeshi Sudan Kusini ameunda vugu vugu jipya la kundi la waasi.
Paul Malong ambaye alitimuliwa katika wadhifa wake na Rais Salva Kiir mwaka, amechukua hatua hiyo wakati nchi yake ikianza tena mazungumzoa ya amani mjini Addis Abba Ethiopia.
Mazungumzo hayo pia, yana lenga kufikia makubaliano ya kuachiliwa kwa Makamu Rais Riek Machar ambaye kwa sasa yuko katika kizuizi cha nyumbani nchini Afrika Kusini.
Malong amekuwa akiishutumu serikali kwa rushwa na makosa ya kuifilisi nchi, anasema kuwa kundi lake la waasi litakuwa na jukumu kubwa la kuiondoa Sudan Kusini kwenye sintofahamu na kuielekeza katika demokrasia na maendeleo.
Wapiganaji Sudan Kusini, na silaha hatariHaki miliki ya pichaREUTERS
Kufuatia kuundwa kwa kundi jipya la waasi, serikali ya Suda Kusin haijasema neno lolote, ambayo inapigana na vikundi kadhaa vya waasi nchini mwake .
Inaarifiwa kuwa wakati Malong alipokuwa ana wadhifa wa mkuu wa majeshi alikuwa akituhumiwa na Umoja wa mataifa kwa kuratibu mashambulizi ya kikabila dhidi ya raia.
Wakati hayo yakijiri inaarifiwa kuwa mapigano yanaendelea nchini Sudan Kusini baina ya vikosi vya serikali na vikundi vya waasi licha ya mpango wa amani uliosainiwa mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment