Akizungumza na MCL Digital leo Aprili 10, Safina amesema lengo lake lilikuwa si kumdhalilisha mtoto ila kuhitaji matunzo.
"Nasikitishwa kuona mwanangu anasambazwa kwenye mitandao, anazo haki na ni mtoto kama watoto wengine," amesema.
Safina amesema mumewe Zhou Quin aliondoka nchini baada ya kibali chake cha kufanya kazi nchini kuisha mwaka mmoja uliopita, hakuna mawasiliano.
Amesema mtoto wake amekuwa akisumbuliwa na magonjwa ikiwamo macho hivyo hana mtu wa kumsaidia malezi.
"Huyu mwanaume anaishi Jiangsu huko China, binafsi sina kazi wala chochote nimekuja kuomba msaada, nisaidiwe mwanangu apewe matumizi," amesema Safina.
No comments:
Post a Comment